Hoja kuhusu wanaotoa 'sadaka' ya fedha.

Hoja kuhusu wanaotoa 'sadaka' ya fedha.

Mphamvu

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2011
Posts
10,702
Reaction score
3,319
Si lengo la bandiko hili kuchukua sura ya kidini, lakini mara kadhaa nimeona watu wakienda katika nyumba za ibada kupokea sadaka kutoka kwa watu wenye uwezo. Wakati fulani nikiwa shule ya msingi tulikuwa tukitoroka kwenda kwa mama mmoja wa Kihindi kuchukua Sh.100 za msaada. Hadi leo ipo baadhi ya misikiti matajiri fulani hutoa fedha kwa kila muumini anayekuja kuswali siku ya Ijumaa.

Hoja yangu inawalenga hasa hawa matajiri wawezeshaji wa fedha, ya kuwa kwanini wasitafute mbinu nyingine ya kuwawezesha hawa watu 'masikini' kuliko kuwapa fedha mkononi? Kawaida hii inaendeleza umasikini wa fikra, hufika hatua ya watu kukopa na kuahidi kuwa ikifika siku fulani nitalipa (kwa kuwa ana uhakika wa kupokea hii sadaka).

Wanaotoa wanaweza kuwa na nia tu ya kutimiza wajibu wao kiimani, kwa kuwa imani nyingi husema tuwasaidie wenye shida lakini nina shaka na aina hii ya usaidizi. Wapo watu wabunifu lakini wanakwama kwa kukosa mitaji pamoja na kuwa mawazo yao ni murua kabisa. Kwanini watoaji hawa wasielekeze nguvu huko kuliko kumpa mtu fedha taslimu, ambayo hajaitolea jasho na inazidi kumtia umasikini?

Naombeni mrejesho.
 
Kwa nini wabuni njia nyingine wakati waombaji wenyewe wanataka fedha?.Kwa kuwa mawazo na akili za mwombaji zipo kwenye fedha kuwapa wazo jipya itakuwa ni kupoteza muda maana hiyo inahitaji waombaji wapewe elimu hiyo.Hata Mungu humpa mtu haja ya moyo wake vinginevyo akikupa tofauti unaona kuwa hajakupa.Mf. Waweza omba utajiri,ukapewa afya njema badala yake,will you recognize kuwa umepewa ulichomba kwa kupewa mbdala?Mtu hawezi kuomba samaki halafu apewe nyoka au aombe mkate apewe jiwe.Aliyeomba fedha anapewa fedha.
 
Wito si kwa hawa watakaji wa fedha, bali watoaji. Wao wana nia ya kutimiza ibada ya sadaka, sio? Kama kuna namna njema zaidi ya kutimiza fungu hili na yenye manufaa zaidi kwanini wasitumie hiyo?

Back
Top Bottom