Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Rais anapotoa ahadi katika kipindi cha miaka 5 ya kwanza na asizitimize katika kipindi husika asiruhusiwe kugombea kipindi cha miaka 5 inayofuata! Hoja hii iingizwe kwenye Rasimu ya Katiba Mpya. Mnaonaje hii wakuu? Nawasilisha kwa mjadala!
Mkuu hiyo haitoshi. Kwa pendekezo hilo kuna uwezekano wa viongozi kuwa very sincere katika kipindi cha kwanza cha uongozi lakini wakawa mbwa mwitu wanapofanikiwa kwa kipindi cha pili. Wanaweza kufanya mambo ya ajabu mno pengine hata kulitumbukiza taifa katika hatari kubwa zikiwapo za kiusalama na kiuchumi kama madeni makubwa yasiyolipika, n.k.
Nadhani hakuna haja ya kuzunguka mbali, Katiba iainishe suala la haki elimu ya uraia; elimu ambayo itasaidia wananchi kuchagua viongozi (wabunge) wazalendo kwa taifa; wabunge watakomchagua Spika kwa uzalendo bila shinikizo za kisiasa, wabunge watakokuwa tayari kulitetea taifa ikibidi hata kwa damu. Na Bunge la aina hii litakuwa na uwezo wa kumuondoa madarakani Rais pale itakapoonekana hatimizi ahadi zake iwe ni kipindi cha kwanza au cha pili.