Zanzibar 2020 Hoja mbili za Membe zawakonga moyo wazanzibari

Zanzibar 2020 Hoja mbili za Membe zawakonga moyo wazanzibari

Missile of the Nation

JF-Expert Member
Joined
May 24, 2018
Posts
15,101
Reaction score
56,054
Katika mkutano wa mapokezi ya wagombea urais kwa tiketi ya ACT, mheshimiwa Membe alipewa dakika chache tu za kuwasalimia wazanzibari, katika dakika hizo Membe aliongea mambo mawili ambayo yaliwafurahisha sana Wazanzibari nayo ni
1)Mamlaka ya nchi ya Zanzibar ndani ya muungano

2) Kuwarudisha masheikh waliotoroshwa na kuwekwa "Kizuizini" huku Tanganyika warudishwe Zanzibar wakahukumiwe kwa sheria za Zanzibar

Hayo mambo kwa kweli yaliwafurahisha mno Wazanzibar.

Kitu kimoja ambacho nimejifunza kwa Membe ni kwamba, kwanza huyu jamaa ni bingwa wa Issues, ukimpa nafasi ya kumsikiliza anakata issues kwelikweli. Ukimpa nafasi ya kumsikiliza lazima akubadili mtizamo!

Pili huko zamani tulikuwa hatujui kuwa kumbe Membe pia ni mtaalamu wa kushambulia jukwaa na kutema cheche kwa convincing power ya kutisha, Kwa kweli uchaguzi huu umetusaidia kumjua huyu jamaa kuwa kumbe siasa anazijua!

Mimi binafsi roho yangu ni nyeupe imetulia tuli kwa uwepo wa Lissu au Membe, yeyote kati ya hao wawili kwangu mimi binafsi anafaa, Nangoja nisubiri maamuzi ya ushirikiano ya wapinzani

Msikilize Membe hapa chini akitema moto huko Zanzibar!

Mkuu hiyo haijakaa vizuri, kwahiyo JK ndio alikataa?

Haijakaa vizuri kivipi? , kuna mambo yanaongelewa ndani ya baraza la mawaziri na ni siri.

Sasa utajuaje kuwa Membe alishauri au hakushauri kwenye hivyo vikao?
 
Sawa mkuu, kwahiyo baada ya kutoka ccm siri ndio imefikia mwisho?!

Ameongea in such a way kuiframe kama policy issue pindi akichaguliwa kuwa rais, hajazungumza as if anatoa siri kuwa amewahi kushauri huko nyuma ushauri wake ukakataliwa, angeongea hivyo angeonekana ni mtovu wa collective responsibility, nami ningemshangaa kwa kweli!

Kugombea urais ni muda wa kunadi kile unachokiamini, ulichokisimamia sirini na dhahiri bila kuvunja dhana ya collective responsibility.

Huwezi kuanza kusimama majukwaani ukasema kuwa nilipokuwa waziri nimewahi kumshauri rais asifanye kadha wa kadha lakini hakunisikiliza, ukisema hivyo utakuwa hufai wewe!
 
Ameongea in such a way kuiframe kama policy issue pindi akichaguliwa kuwa rais, hajazungumza as if anatoa siri kuwa amewahi kushauri huko nyuma ushauri wake ukakataliwa, angeongea hivyo angenekana ni mtovu wa collective responsibility, nami ningemshangaa kwa kweli!

Kugombea urais ni muda wa kunadi kile unachokiamini, ulichokisimamia sirini na dhahiri bila kuvunja dhana ya collective responsibility.

Huwezi kuanza kusimama majukwaani ukasema kuwa nilipokuwa waziri nimewahi kumshauri rais asifanye kadha wa kadha lakini hskunisikiliza, ukisema hivyo utakuwa hufai wewe!

Duuu, haya kaka.
 
Ameongea in such a way kuiframe kama policy issue pindi akichaguliwa kuwa rais, hajazungumza as if anatoa siri kuwa amewahi kushauri huko nyuma ushauri wake ukakataliwa, angeongea hivyo angeonekana ni mtovu wa collective responsibility, nami ningemshangaa kwa kweli!

Kugombea urais ni muda wa kunadi kile unachokiamini, ulichokisimamia sirini na dhahiri bila kuvunja dhana ya collective responsibility.

Huwezi kuanza kusimama majukwaani ukasema kuwa nilipokuwa waziri nimewahi kumshauri rais asifanye kadha wa kadha lakini hakunisikiliza, ukisema hivyo utakuwa hufai wewe!

Unaweza kuona aina ya raia tulionao na uelewa wao. Hawezi kukuelewa kwa uRais. Ni uelewa huu mdogo ndio hautambui mahitaji yetu kama taifa. Ustawi wa jamii kwao ni jambo lisilo na msingi zaidi ya flyover Tazara. Wanaodhani uchaguzi ni zawadi kwa mambo mazuri ya zamani na sio kitu forward-looking!! Ndio maana tunasikia uchaguzi kwa kuangalia vitu vya nyuma. Jamaa anazungumzia “siri za baraza la mawaziri kabla ya 2015”. Badala ya kuzungumzia “washitakiwa warejeshwr Zanzibar kwa sababu kama kuna makosa waliyatenda wakiwa Zanzibar na Zanzibar ina sheria zake”.
 
Ukiona wanazidi kuvibana vyombo vya habari visirushe habari za wapinzani, ujue wameshikwa pabaya!

Lissu anyooke hadi Rusumo kisha Kagera.

Huko pana barabara ambazo kwa hakika kuna samaki haihitaji mafuta kuwakaanga. Samaki wenyewe wamenona vilivyo:

Lissu tembelea Rusahunga - Rusumo haraka iwezekanavyo

Chini katika picha ni ajali ya leo, sababu: ubovu wa barabara usiomithilika:

IMG_20200810_152339_062.jpg

Chini katika picha hii ya leo, ni watoto wanaoomba mia mia kwa kuziba mashimo badala ya kwenda shule:

IMG_20200810_152548_190.jpg
 
Hao viongozi wa dini kweli wote wazima kwa mujibu wa maneno ya Mhe. Membe?
 
Back
Top Bottom