HOJA NDANI YA HOJA: Rais Magufuli na bahati nasibu ya korona - ITALIPA?

Sisi tumefuata njia ipi kuokoa raia wetu wanaopukutika?

Unaweza kutoa ushahidi kwa hao raia wanaopukutika? BTW kama unao huu ugonjwa njoo utibiwe kwenye Hospitali zetu upate Madagasca cure. Wacha kuwewesekaweweseka.
 
Mkuu, siasa zetu ni mbaya Sana, za kusubilishana kweny korido na kuombeana mabaya,

Kwa sababu, kile ambacho kinachosemwa na wapinzani kinaweza kuwa kweli ama sio kweli

Unajua mkuu, Corona ipo kweli na kila mtu anakili hivyo, Corona ambayo ipo ukiacha mihemko na joto la kisiasa nchini, ukaamua kujifanyia uchunguzi wa kwako bila kuiachia mitandao ifanye uchunguzi halafu ilete, unaweza ukajikuta unaogopa kiasi kwamba kuutoa mguu wako kwenda mahali ni lazima ururudi na mahututi na maambukizi ya Corona

Mfano mdogo Kaka hapa ni kwamba, tunajua CVD haina itikadi, inavamia na kuua yeyote, na tumeona jinsi ambavyo utendaji wake huko ng'ambo kiasi kwamba kule ni kama pembe la ng'ombe halifichiki, utangaze usitangaze, wananchi watashuhudia Tu wimbi kubwa la miili ya watu wakiwa wamekufa

Utofauti uliopo hapa kwetu, wengi wetu, kila mmoja anajiongelesha tu akiwa hana hata ushahidi wa vifo vingi mitaani

Ni kila mmoja anaandika kuleta nyuzi akitegemea apate ukweli wa wapi watu ambao anadai wengi wanakufa, wengi wa wandishi hapa ndicho wanachotegemea, lakini Wao kama Wao hawana ushahidi hata kidogo

Angalia hata hao wanaoandika kila leo kudai kuna vifo vingi nchini, tangu Corona imeingia wamebaki kuwa ni haohao, unajiuliza, kama ni vifo ni vingi si lazima pia kuna maambukizi mengi? Lakini Kwa nini kila leo tunaona kila mtu hapa akiendelea kuchangia michango hapa, inamaana watu ambao wamejisajili ktk mitandao ya kijamii, Corona inawaogopa?

Ni Nani anayestahili kuugua na kufa Kwa ugonjwa wa Corona?

Ukitaka kupata ukweli juu ya ugonjwa wa Corona, usisubiri mitandao ikuletee ukweli, maana mitandao ya kijamii yetu hapa imetawaliwa na siasa, ni siasa Tu hata kwenye mambo yasiyohitaji siasa,

Kwa hiyo, hii bahati na sibu ya Magufuli, huenda ikatiki hasa kwenye eneo la njia alizoamua kuzitumia kupambana na Corona, zinaweza kumpa ushindi, kama si Leo basi kesho,
 
So far amechangia nini!?? Anayepaswa kuwalinda Watanzania wote amefanya nini?
Usitafute kiki ya kisiasa kwenye Janga hili.
labda nikuuluze so far umechangia nini kigoma ujiji ili kuwalinda wapiga kura kwa janga hili?
 
"paul sylvester, post: 35378925, member: 587771"]Utofauti uliopo hapa kwetu, wengi wetu, kila mmoja anajiongelesha tu akiwa hana hata ushahidi wa vifo vingi mitaani
Kwa wenzetu ili kuwa na uhakika na takwimu kila siku kuna mamlaka inatoa. Hilo linapunguza habari au taarifa zisizo rasmi.
Kwanini hapa nyumbani serikali haitaki kutoa takwimu? Kama hakuna takwimu kwani watu wenye hisia zao walaumiwe? Mtu akisema waliokufa hadi sasa ni 5,000 atakuwa amekosea nini? Kwa maana kwamba takwimu zinapingwa na takwimu, sasa kama hakuna takwimu za serikali ambazo ni za uhakika na rasmi, nani alaumiwe?
Kwanini watu wanazikwa usiku na si mchana, na kwanini wanazikwa chini ya uangalizi? Ikiwa mtu kafariki kwa ugonjwa mwingine na si Corona kwanini azikwe chini ya uangalizi?
Ni kila mmoja anaandika kuleta nyuzi akitegemea apate ukweli wa wapi watu ambao anadai wengi wanakufa, wengi wa wandishi hapa ndicho wanachotegemea, lakini Wao kama Wao hawana ushahidi hata kidogo
Kwanini watu wanazikwa usiku chini ya uangalizi? Kwanini serikali inashiriki mazishi ya watu siku hizi na si kama ilivyokuwa utamaduni wetu? Takwimu rasmi zitoke wapi? Kwanini imezuliwa kutoa takwimu rasmi? Nani anahusika kutoa takwimu rasmi na kwanini hazitolewi tena? Yuko wapi Ummy na kwanini kakaa kimya?Ulimsikia Mwigulu?
Ukitaka kupata ukweli juu ya ugonjwa wa Corona, usisubiri mitandao ikuletee ukweli, maana mitandao ya kijamii yetu hapa imetawaliwa na siasa, ni siasa Tu hata kwenye mambo yasiyohitaji siasa,
Hatutaki kusikia EAC, SADCC au WHO halafu tunalaumu mitandao!
Kwa hiyo, hii bahati na sibu ya Magufuli, huenda ikatiki hasa kwenye eneo la njia alizoamua kuzitumia kupambana na Corona, zinaweza kumpa ushindi, kama si Leo basi kesho,
Kwa aliyepoteza ndugu na aliyepata uchungu neno bahati nasibu ni tusi kwake. Huwezi kucheza bahati nasibu katika nafsi ya mwanadamu. Bahati nasibu inachezwa na makorokoro mengi si roho ya mwanadamu na hakuna kufanikiwa kwa bahati nasibu hasa kwa wanaopoteza ndugu kila siku na kuzikwa usiku chini ya usimamizi.
 
Unajiandikia kitu usichojua. Ni watu wengi wamefariki ambao wangeweza kupona kama hatua zingechukuliwa. Lawama zote anabeba rais kwa kuamua kufuata njia za kijima badala ya kisanyansi. Watu wamefariki wengi, Magufuli ameitumbukiza nchi shimoni.
 
"Mfumo wa afya wa Tanzania unaweza kujikuta ukiporomoka kuliko tunavyoweza kudhania. Tumeona jinsi nchi za daraja la kwanza (Italia, Ufaransa, Marekani na China) zikipata shida kukabiliana na ugonjwa huu. Imefikia mahali serikali za nchi hizo zimeomba na zinategemea misaada kutoka makampuni binafsi kupata dawa na vitendea kazi mbalimbali. Kuna hospitali Marekani manesi wake walijikuta wakitumia mifuko ya plastiki ya takataka kama mavazi ya kujikina! Marekani hiyo! Tumeona Hispania, wazee wakiachwa wajifie wenyewe kwani manesi na wahudumu wengine wamekimbia! Tumeona Italia madaktari na manesi wakifa kutokana na ugonjwa huu. Kama hili linatokea kwa mti mbichi, itakuwaje kwa mti mkavu! Kama limetokea kwa chuma cha pua, itakuwaje kwa chuma chakavu!"

Kwa maelezo hayo nadhani bahati nasibu ya Magufuli imelipa au mnasemaje?
 
JPM ametoka kidedea, wana JF pamoja na kumponda, hivi sasa wanaishi kwa amani bila Covid 19.
 
JPM ametoka kidedea, wana JF pamoja na kumponda, hivi sasa wanaishi kwa amani bila Covid 19.
Hivi akili za kawaida tungebaki ndani (lockdown) au hivi ilivyo, maisha yangesimama hama yangeendekea ila katika mfumo tofauti?
 
Kuna kitu kimejificha hapa! Kuna hujuma inafanyika kuleta hofu kwa watanzania! Rais wetu mpendwa Mh Dr JPM alishasema kuwa tutatishwa ili tuikubali chanjo! Mungu azidi kumlinda kumuongoza na kumbariki rais wetu mpendwa Mh Dr JPM na serikali yetu yote! Mungu azidi ibariki Tanzania!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…