Katiba iliyopo ni katiba ya kimungu mtu.
Ni katiba bora sana kwa watawala na mawakala wao na vibaraka wao.
Katiba iliyopo siku moja itakuwa katiba bora sana kwa watawala wezi,mafisadi ,wahalifu na wavunja haki za kibinadam.
Katiba iliyopo itakuwa katiba bora siku moja kwa wanyanyasaji alimradi tu wawe madarakani.
Katiba iliyopo itakuwa katiba bora sana kwa viongozi wa aina zote hata hata wale wasiokuwa na nia njema na taifa letu wanaweza pia kuitumia na kutimiza malengo yao bila kuulizwa.Wengi walitumia madaraka vibaya kupitia katiba hii inayolinda watawala na kukandamiza haki za wananchi.Hata waliotuhumiwa kufisidi mali za umma ni kwa kutumia udhaifu wa katiba iliyopo.
Katiba iliyopo ni katiba bora kimadaraka na kugawana vyeo vyenye maslahi manono.
Katiba iliyopo inaweza kutumika vibaya kukandamiza haki za makundi mbalimbali katika jamii kama vile:-
Dini,waandishi wa habari, wabunge, wananchi wa kawaida,wakulima,wafugaji,wafanyakazi, wafanyabiashara,wanasiasa ,watoto n.k
Ni katiba yenye tabaka kubwa sana kati ya watawala na watawaliwa.
Hii katiba iliyopo itakua ni katiba bora siku wakitokea au akitokea mtawala anayeendekeza udini au ubabe au ukabila au ufisadi.
Mana kuna siku atatokea mdini mmoja akaamua kuweka serikali ya dini yake kuanzia mawaziri wote ,wakuu wa mikoa wote,wakuu wa wilaya wote,mabalozi ,wote,wakurugenzi wote,wabunge wa kuteuliwa wote ,makatibu tawala wote,wakuu wa idara wote,wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama wote ,yaani kila sehem na hakuna wa kumuuliza na ukimuuliza unatiwa misukosuko iwe fundisho kwa wengine na wateule wake wote watasimama na kumtetea kwa nguvu zote.Vyombo vyote vya habari vitaongea lugha ya mkubwa.
Hapo pia tutaambiwa tusubiri maendeleo na sio kuleta hoja za udini wameteuliwa kwa sifa na sio dini zao.
Hii ni katiba bora kabisa siku moja akitokea mtawala Mkabila. Atateua kabila lake kwenye nafasi zote za uteuzi na hakuna wa kumuuliza.Atakayehoji utasikia pyuu pyuuu.
Kikwete alitembea sana duniani na alijifunza mengi hakuwa mjinga kukubali mchakato wa katiba mpya. Angekuwa mbinafsi na mhalifu asingekubali mchakato wa katiba ambayo ilikuwa inatoa mamlaka ya kumshitaki yeye mwenyewe. Hii inadhihirisha wazi kuwa JK alikua mtu safi na alitaka kutuachia misingi ya usafi kupitia Katiba.
Na wakati wa mchakato huo madaraja makubwa yalikua yakijengwa na sio hayo tu na barabara za lami nchi nzima, majengo bora ya kuushi kwa wapiganaji wetu wa jeshi la wananchi na wakiongezwa mishahara na watumishi wote nchini huku wafanyabiashara wakinawirisha na kupanua biashara zao. Wawekezaji wakiongezeka na viwanda vikubwa vikijengwa kwa kasi.
Makusanyo ya kodi yalifikia bilioni mia tisa na zaidi kwa mwezi, mzunguko wa fedha ukiwa mkubwa kwa wananchi.Wananchi wa kawaida wakijitahidi kujenga nyumba bora vijijini vijijini . Wasanii na wachezaji nao wakizidi kuwa na maisha bora.
Ni wakati pia ambapo Ajira za umma na binafsi zikizidi kushamiri.Udahili wa Wanafunzi wa Elimu ya juu uliongezeka.
Demokrasia na Elimu ya siasa na haki za binadamu ulikuwa unazidi kukua. Mawaziri wengi waliotuhumiwa kwa ufisadi walifukuzwa.Ndio wakati hasa ambapo cheo kilikua sio mali ya mtu bali dhamana.
Kipindi hicho waliibuka vijana wengi machachari kisiasa ambao leo wana majina makubwa na nafasi kubwa kwenye vyama na serikali.
Vyombo vya habari vya kutosha mpaka vijijini.
Haya ndio maendeleo endelevu duniani kote.
Hayo maendeleo ya vitu yalifanyika enzi za wakoloni mana waafrika walikuwa wanahesabika sawa na wanyama wasio na thamani yoyote kutokana na kutokuwa na elimu kabisa na pia umaskini na ufukara wa jamii kubwa ya kiafrika.Walikandamizwa na kuporwa haki za utu wao kwa kutumia katiba kama tuliyo nayo leo.
Watu wasio na elimu ya kutosha na maskini ndio wanaotumiwa na wasomi wachache wanaotawala kunufaisha kundi dogo la watawala na wanasiasa.
Kwa sasa tunahitaji kuongozwa sio kutawaliwa na ndio ulikua msingi wa kupigania uhuru toka kwa wakoloni.
Tunataka katiba mpya unayoondoa viashira vyote vya watawala kuwa na hulka zile za wakoloni kwa sababu tu ya kubaini kuwa kuna kundi kubwa la watu wasio na elimu yakutosha na maskini.
Katiba mpya na bora haizuii maendeleo bali inaweka misingi imara na ya wazi ya usimamizi wa maendeleo hayo.
Tunawakumbuka na kuwaenzi mitume na manabii watakatifu na watukufu sana sio kwa sababu walitujengea mabarabara au majumba na miundo mbinu mizuri la hasha . Tunawaenzi kwa sababu walituachi misingi ya sheria na miongozo ya kufuata kama dira ya maisha ya kila siku.