rose mzalendo
Member
- Mar 5, 2019
- 71
- 114
Nimesikiliza kwa makini hotuba ya mgombea Urais kwa tiketi ya Chama cha NCCR-Mageuzi Bw. Jeremia Mganja akinadi sera zake kwa Wananchi. Hotuba yake inatoa taswira ya tabia za wagombea wa vyama vya upinzani kuwa wamezoea kupotosha jamii. Wamesahau kuwa Watanzania kwa sasa wana uelewa mkubwa wa kuwapima kwa kuwasikiliza na kuzichambua sera zao.
Hapa nitachambua mambo matano aliyoyaainisha kama ifuatavyo;
(1) Katiba
Katika kipengele hiki Bw. Mganja amefanya upotoshaji huku akijua fika Katiba tulionayo haijatupungukia na imekuwa ikifanyiwa marekebisho ya kisheria na kikanuni ili kuendana na mazingira na wakati tulionao kwa sasa. Hadi ninapoandika waraka huu Katiba ya Jamhuri ya Muungano imeshafanyiwa marekebisho mara tatu. Swali la kujiuliza ni kuwa Mganja anapata wapi uthubutu wa kutuambia Katiba yetu ni ya kikoloni na inatoa mwanya kwa chama kilichopo madarakani kuwa na Serikali ya kiutawala badala ya Serikali ya kiutendaji.
(2) Polisi
Japokuwa Bw. Mganja anataka kuongoza nchi lakini hana uelewa wa majukumu ya Jeshi la Polisi ambalo ataliongoza, vinginevyo awe ameamua kupotosha kwa makusudi ili kupata umaarufu maana najua hawezi kuwa Rais wa nchi hii. Mganja anapaswa kujua kuwa Jeshi la Polisi lina jukumu la kulinda Raia na Mali zao. Ni ujinga wa kiwango cha juu kwa Mganja kuongelea Jeshi hilo nje ya majukumu yake, ikizingatiwa kuwa mpaka anapata jeuri ya kutembea na kuendesha shughuli za kampeni kwa usalama ni kutokana na utekelezwaji mzuri wa majukumu ya Jeshi la Polisi. Watanzania sera hizi ni za kupuuza na zimejaa upotoshaji maana Mganja hivyo alivyo hadi sasa tegemeo lake na kimbilio lake ni Polisi anaowashambulia.
(3) Ukabila
Mganja anathubutu kuzungumzia Ukabila na hata *chama chake* kimekuwa kikikumbatia ukabila wakati anakumbuka vyema jinsi muasisi wa Taifa hili Mwl. Julius Kambarage Nyerere alivyokuwa hataki kabisa kusikia mtu hasa Mtanzania akimtaja mwingine kwa kuuliza kabila. Huyu Bw. Mganja alipatwa na nini kilichomsukuma kuongelea makabila na mbaya zaidi akilisifu kabila analotokea kuwa ni la kikatili na jeuri huko Musoma. Ni dhahiri huyu mgombea amelelewa na kukulia katika misingi ya ukabila au familia inayokumbatia ukabila. Watanzania wenzangu wagombea wanaoongelea ukabila katika kampeni na sera zao ni wa kuwaogopa kama ukoma, hawatufai kabisa.
(4) Nchi yetu siyo masikini
Kauli hii ya Bw. Mganja ni sahihi na inawezekana akawa mpinzani wa kwanza au wa pili kukiri hili, vinginevyo neno tumekuwa tukilisikia zaidi kutoka kwa Mgombea wa CCM JOHN POMBE MAGUFULI. Hata hivyo tofauti zao ni kuwa Magufuli amekuwa akilisema na kueleza mikakati ya kuifanya nchi kuwa tajiri lakini huyu jamaa Maganja hajawahi hata kusikika akitoa mawazo tu ya mikakati itakayoipeleka Tanzania mbele kutokana na ujajiri uliopo.
Tumeona hatua na juhudi kubwa zikifanywa katika kipindi cha miaka 5 ya uongozi wa MAGUFULI. Amethubutu kuanzisha miradi mikubwa ya kimkakati katika kukuza uchumi na imesaidia Taifa letu kupaa kiuchumi na kuzifanya Taasisi za Kifedha Duniani kuitambua Tanzania kuwa nchi yenye uchumi wa kipato cha kati. Hakika si kwamba Bwana Mganja haoni maendeleo ya Nchi hii kwa kipindi cha miaka 5 bali ameamua kupotosha ili kujipatia umaarufu tu maana anajua hana uwezo wa kushindana na Magufuli.
(5) Maovu
Bw. Mganja katika hotuba yake amejaribu kutengeneza ushawishi kwa Watanzania kuwa kila linalofanyika kwa manufaa ya nchi ni Uovu, hili linahitaji kuwa na kichaa cha kifafa uweze kukubaliana nae. Watanzania tayari tuna imani na mgombea wa CCM kutokana na utendaji kazi wake pamoja na utumishi uliotukuka, hakika Magufuli tumepewa na Mungu. Mfano mzuri tumeweza kukombolewa kipindi cha janga la ugonjwa wa KORONA ambapo tulimshuhudia Magufuli akikabidhi nchi kwa Mungu alipowataka Watanzania kufunga na kuomba kwa siku tatu.
Wito kwa Wananchi tunapaswa kusikiliza sera za vyama vyote tuzichambue na kuhakikisha hatukosei tarehe 28 Oktoba, 2020 kwa kumchagua *MAGUFULI*. Kwa sasa Watanzania tunataka kiongozi mwenye uchungu na rasilimali za nchi kwa manufaa ya watanzania na si mabeberu.