Maoni haya hayana mantiki yeyote; kwani hatua ya kwanza inayotakiwa kuchukuliwa ni kuibana serikali ili iweze kukubali kwa dhati kuanzisha mchakato wa kutunga katiba mpya. Baada ya hapo, serikali inapashwa kuonyesha utayari wake wa kukubali mabadiriko ya katiba kwa kuongoza mashauriano na vyama vya siasa na vya kijamii ili kubuni njia muafaka inayoungwa mkono na makundi yote hayo, itakayofanikisha upatikanaji wa katiba hiyo.