Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,771
- 41,027
[h=5]Kama kuna mtu yeyote anayejua anisaidie; ni wapi katika Katiba ya sasa ambapo Rais au mtu yeyote yule amepewa madaraka ya kuanzisha mchakato wa kuandika Katiba Mpya? Ikumbukwe kuwa viongozi wote walioanzisha mchakato wa kuandika Katiba Mpya waliapa "kuitetea, Kuilinda, na kuihifadhi" Katiba ya sasa![/h]Fikiria kuwa walipoanzisha huu mchakato wa kuandika "Katiba Mpya" walifanya hivyo kwa matakwa yao tu. Hakukuwa na hoja Bungeni, hakukuwa na kikao cha Kamati Kuu ya CCM na wale hakukuwa na utaratibu ambao ulikuwa unafuatwa. Cha kushangaza hata hivyo ni kuwa waliposema wanakubali kuandika Katiba Mpya (kinyume na Katiba ya sasa) wakasema baadhi ya mambo yaliyomo ndani ya Katiba ya sasa hayawezi kuhojiwa na wananchi! Kwamba wananchi wanaweza kuzungumzia mambo mengine yote isipokuwa mambo fulani fulani! Nani aliwapa madaraka ya kuamua nini kisizungumzwe? Walipata wapi madaraka ya kuwakataza wananchi wasijadili na kuamua baadhi ya mambo kwa mfano uwepo wa Jamhuri ya Muungano?
Ndio maana nasema ingekuwa nchi nyingine...
Lakini kwa vile hii ni Tanzania....
Ndio maana nasema ingekuwa nchi nyingine...
Lakini kwa vile hii ni Tanzania....