Chadema inataka Katiba Mpya na Tume Huru ya Uchaguzi
Hapa ndipo mvua itakapoanza kuwanyeshea kama hamtakuwa makini sana.
Mtaanza kuwa kama mnababaika na hamjui nini la kufanya. Leo hili, kesho lile.
Mliweka msimamo ulioeleweka huko siku za nyuma, kwamba hapatakuwepo na uchaguzi wowote bila Katiba Mpya, na Tume huru ya Uchaguzi.
Mlitakiwa kushikilia hapo hapo na kuliwekea uzito mahali popote kwenye mikutano yenu, ili wananchi wasiwe na mashaka yoyote juu ya msimamo wenu.
Mwenyekiti alipoanza kuyumba, chama kikaanza kuwa na mashaka na adhimio lile.
Tukawaeleza Samia swala la Katiba Mpya kisha lizima, nyinyi hamkuelewa!
Kitakachowasaidia sasa ni hili la Bandari, mkiliunganisha vizuri na hayo matakataka mengine wanayofanya CCM, hata chini ya Katiba hii iliyopo CCM hawatoboi.
Mtasema Katiba hii inamfanya Rais awe mungu. Huyu mungu hawezi kushindana na nguvu za wananchi wakishawaelewa na kuamua kuwaondoa CCM.
Kumbuka, ni CCM watakaoanza vurugu, hata uchaguzi ukifanyika chini ya hii Katiba iliyopo. Anayefanya vurugu ndiye atakayedhibitiwa.
Sasa nawaomba, acheni kuwachanganya akili wananchi. Ni lazima msimamo wenu uwe wazi kabisa, wananchi na dunia yote ijue hivyo.