Muarobaini Mchungu
JF-Expert Member
- Apr 9, 2013
- 281
- 54
Bunge letu la katiba linaelekea kutoa picha halisi ya ni jinsi gani watanzania tulivyo zaidi ya kuonyesha au kusaidia kuipata katiba mpya kama wote tulivyonuia. Ushabiki wa vyama na sera za vyama zimejionyesha wazi na hata wajumbe kuanza kujadili/kuanzisha hoja za nguvu huku wakishindwa kuzijadili na kuacha nguvu ya hoja ichukue nafasi.
Ni ukweli usiopingika kuwa hakuna asiyekuwa na upande au mshabiki wa chama fulani miongoni mwa wabunge lakini wanashindwa kujizuia na kujadili hoja kwa manufaa ya Tanzania. wamebakia kujiuliza nani kaleta hoja...ccm?au Chadema? au... zaidi ya kuijadili ile hoja kwanza. Wote tunajua atakacho kisema Lisu huenda ikawa asilimia kubwa ni mawazo au matakwa ya Chadema, vivyo hivyo kwa atakayosema Pinda kiasi kikubwa yataiwakilisha ccm. Swali ninalojiuliza ni je Mazingira hayo yanakwepeka? kama hayakwepeki kitu ambacho ndio ukweli wenyewe basi ningeshauri yajadiliwe, wabunge wapeane nafasi sio kuzomeana!
Leo nimesoma habari zikisema mbowe alaani tabia ya kuzomeana bungeni!!! ilinistua kidogo.....nikataka kurudi nyuma kwenye yaliyokuwa yakitokea katika bunge la Tanzania siku chache zilizopita.. lakni nikaendelea kuisoma hoja yake na ni ujumbe tosha kwamba hoja zijadiliwe, zikubaliwe au zikataliwe kwa ustaarabu kwani mwisho wa siku tunajenga nchi moja.. Yaani inakera sana, inanikumbusha kipindi fulani upinzania wa simba na yanga.....unakuwa unaletwa hadi kwenye Timu ya Taifa.....kule sie tuna wachezaji kadhaaa au sie hatuna wachezaji so ile sio Taifa stars ila ni Simba au ni Yanga....Upuuzi mtupu....
Kwa hali ilivyo sidhani kama mawazo ya wale wasiokuwa kwenye vyama vya siasa yatajadiliwa....kama sio sera toka miongoni mwa vyama husika... Nawaomba watanzania tutafakari juu ya habari tunazoziona au kusikia na tuwe tayari kuipinga au kuikubali katiba mpya.......