Petro E. Mselewa
JF-Expert Member
- Dec 27, 2012
- 10,307
- 25,932
Hoja hii iliyo katika Rasimu ya Pili ya Katiba iliyokabidhiwa kwa Rais Kikwete na Rais Shein na kutetewa ipasavyo na Jaji Warioba inapotoshwa sana. Inaandamwa na propaganda.Mojawapo ni kuwa na Marais watatu! Nani amesema (au Rasimu gani iliyopendekeza Marais watatu)? Huu ni upotoshaji.
Rasimu ya Jaji Warioba inahusika na suala moja kuu:Serikali ya Muungano. Ni Tanzania tu na si Zanzibar wala Tanganyika. Kwakuwa Rasimu inazungumzia namna Serikali ya Muungano itakavyokuwa,ndiyo maana Serikali za Zanzibar na Tanganyika (iliyoitwa Tanzania Bara) zinadokezwa. Mantiki hapa ni kuwa Tanzania itakuwa moja lakini yenye Serikali tatu. Moja ni zao la muungano (Serikali ya Muungano).Ya pili ni Serikali ya Tanzania Bara (kama mshiriki wa muungano) na Serikali ya Zanzibar(mshiriki mwingine wa muungano).
Kinachozaa propaganda zote hizi dhidi ya serikali tatu ni Urais. Vipo vyama na watu wenye 'airtime' kwenye vyombo vya habari na Serikalini waliojaa mawazo ya 'Urais' tu. Wakilala-urais;wakiamka-urais. Wanapotosha hoja kwa kusema kuwa Tanzania itakuwa na Marais watatu. Si lazima kuwa na Marais watatu. Mbona Ujerumani yenye Serikali za Majimbo 16 haina Marais 17? Marekani kuna utawala wa aina hiyo hiyo lakini Rais mmoja.
Hakuna hata Ibara moja ya Rasimu ya Tume ya Jaji Warioba inayopendekeza muundo wa Serikali za Tanzania Bara na Zanzibar. Wasingeweza kupendekeza hivyo kwakuwa hiyo haikuwa kazi yao.Wao walikuwa kimuungano. Mfumo na ukubwa wa Serikali za Tanzania Bara na Zanzibar vimeachwa kwa wahusika wenyewe. Watafanya hivyo na watakavyo iwapo Rasimu ya Muungano itapitishwa kama inavyopendekeza.
Hakuna hata Ibara moja ya Rasimu ya Tume ya Jaji Warioba iliyopendekeza aina ya viongozi wa Serikali za Tanzania Bara na Zanzibar;kama ziongozwe na Marais,Mawaziri Wakuu,Wafalme au Wakuu wa Mikoa. Hii hoja ya Marasi watatu inatokea wapi zaidi ya kuwa upotoshaji wa Rasimu?
Wengi wetu tunajua,tunatambua na kuthamini kazi ya Tume ya Jaji Warioba. Imewasikiliza watanzania na kuandika maoni yao juu ya Katiba yao katika Rasimu. Wao wameandika tu maoni ya watanzania. Yeyote atakayejaribu,kulazimisha au kushawishi kuchakachuliwa kwa maoni hayo,hatabaki salama. Huo ndio ukweli. Kadiri muda unavyokwenda,ndivyo tunavyoendelea kuwaona wapotoshaji na kujiandaa kuwashughulikia.
Time will tell!