Hoja ya Simba kuitwa Bob Jr, Serikali yasema ‘Simba akiitwa jina la Masanja hakuna atakayemjua’

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
Serikali imesema majina maarufu yanapotumika katika masuala ya utalii mfano kwa Wanyama kama ilivyokuwa Simba aliyejulikana kwa jina la Bob Jr na mwanaye Rihanna ni sehemu ya kujitangaza kimataifa.

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mary Masanja amesema “Tunapotumia majina maarufu tunaitangazia Dunia na si Tanzania pekee, tukimpa jina la Masanja hakuna atakayemjua.”

Hoja hiyo imetolewa Bungen na Mbunge Sophia Mwakagenda aliyeshauri majina ya mashujaa wa Tanzania yatumike mfano Mkwawa, Mwansansu au Mwakatumbula.
 
Ukisikiliza hao viongozi unajua tu kwanini nchi hii tumeachwa na wenzetu toka tulivyopata uhuru, kwanini taifa hili halisongi mbele.

Tuna viongozi vilaza na mapimbi kuliko.
 
Sasa si ndio Masanja angejulikana kupitia Simba.. Simba awatangaze ndugu zetu wasukuma ulimwenguni, sioni ubaya.

Ilichokifanya serikali hapo ni ukoloni mamboleo.
 
Mlitaka Simba aitwe nyerere au Julius ,kwahiyo hayati alikua na Rasta ?

Mtoto wake ,mlitaka aitwe bibi titi Mohamed ,je huyo mtoto wa bob Jr hali ya urembo wake ni kweli unafafa hivyo na bibi titi ?
 
Na nyie nendeni mbugani mkiwaona wanyama muwape majina yenu

Ova
 
Serikali imesema majina maarufu yanapotumika katika masuala ya utalii mfano kwa Wanyama kama ilivyokuwa Simba aliyejulikana kwa jina la Bob Jr na mwanaye Rihanna ni sehemu ya kujitangaza kimataifa.

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mary Masanja amesema “Tunapotumia majina maarufu tunaitangazia Dunia na si Tanzania pekee, tukimpa jina la Masanja hakuna atakayemjua.”

Hoja hiyo imetolewa Bungen na Mbunge Sophia Mwakagenda aliyeshauri majina ya mashujaa wa Tanzania yatumike mfano Mkwawa, Mwansansu au Mwakatumbula.
Hawa wabunge hovyo kabisa
 
Ndio watu wakusoma report ya vitabu vitano vikubwa hawa na kuikaba koo serikali, kama ata taarifa za video tu awafuatilii.

Mbona waongoza utalii mbali mbali wameeleza sababu za Simba kuitwa Bob Junior ni nywele zake za msokoto kama rasta na baba yake pia aliitwa Bob kwa sababu ya nywele.

Halafu umaarufu wake aujatokana na jina tu, ila interaction zake na watalii; yeye alizoea magari ya utalii akiyaona yamesimama anayafuata tofauti na tabia za simba wengine. Matendo yalipelekea kuzoeleka na wageni ndio sababu za kuwa maarufu. Sio jina pekee lililombeba, na tabia zake pia.

Wabunge wengi hasa wa kike kutoka CCM wana midomo mirefu kweli lakini huo muda wa kufuatilia mambo hawana.
 
Daah ukitaka kujua nchi Ina wajinga wengi angalia sampuli iliyopo bungeni!!🤔🤔🤔
 
Nilikuwaga na mbwa wangu mmoja nlikuwa namuitaga masantula

Ova
 
Serikali imesema majina maarufu yanapotumika katika masuala ya utalii mfano kwa Wanyama kama ilivyokuwa Simba aliyejulikana kwa jina la Bob Jr na mwanaye Rihanna ni sehemu ya kujitangaza kimataifa.

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mary Masanja amesema “Tunapotumia majina maarufu tunaitangazia Dunia na si Tanzania pekee, tukimpa jina la Masanja hakuna atakayemjua.”

Hoja hiyo imetolewa Bungen na Mbunge Sophia Mwakagenda aliyeshauri majina ya mashujaa wa Tanzania yatumike mfano Mkwawa, Mwansansu au Mwakatumbula.
Hii nayo ni ya kujadiliwa Bungeni? Sad
 
Back
Top Bottom