Hoja ya waziri Mwigulu Nchemba serikali kuachia Trilion 5 ni absolutely Zero-sum game

Hoja ya waziri Mwigulu Nchemba serikali kuachia Trilion 5 ni absolutely Zero-sum game

Abdul Nondo

JF-Expert Member
Joined
Oct 28, 2016
Posts
520
Reaction score
2,930
Mh @mwigulunchemba hii hoja ya kwamba serikali imekusudia kuingiza au kuachia tsh.trilion tano kupitia kulipa wazabuni wanaoidai serikali ili ziingia katika mzunguko na kwa wananchi, hoja hii na kwa sasa kutokana na makato ya tozo hizi ni absolutely Zero-Sum Game.

Sababu fedha zitakazolipwa hizo trilion 5 zitakwenda kwa watu wa chache kwanza na mzunguko wa fedha hizo inategemea na matumizi ya wanaolipwa (Hao wazabuni) (mfano, wengine wanawezakuzipeleka nje) hivyo fedha hizo hazitarudi katika mikono ya wananchi hata robo ya kiwango kinachochukuliwa na serikali kutoka kwa wananchi.

Mbili, hizo trilion 5 ni absolutely zero sum game sababu hata muuza nyanya akibahatika kupata Tsh.2000 kati ya hiyo trilion 5 ,atakatwa kwenye muamala (itarudi serikalini) badala ya fedha hiyo angeweza nunua unga ili watoto wake wale ila atakatwa , hoja ya kuachia trilion tano ni absolutely Zero -Sum game ni sawa na kutoa mfuko wa kulia na kuweka mfuko wa kushoto katika suruali au shati moja. Na hii l believe itakuwa na Negative Multiplier effect katika uchumi sababu matumizi yatapungua (Fall of consumer spending).

Sio kwamba napinga sisi wananchi kutozwa kodi la, sipingi ila kiwango kilichotozwa ni kikubwa mno.

kulikuwa na sababu gani tozo hii kupigwa mara mbili katika muamala mmoja? yaani (Double taxation/levy in a single transaction) mfano, mtu anamtumia mama yake Tsh. 200,000 ya matibabu kwa tigo pesa, atakatwa Tsh. 4140 (Ada ya Tigo tsh.1,200 na tozo ya Serikali ni tsh.2940) zamani angekatwa Tsh. 1,200 (Ada ya tigo tu), mama yake akienda kutoa anakatwa Tsh. 8340 (Ada ya tigo 5300 na tozo ya Serikali ni 2940) zamani angekatwa 5300 tu , ila sasa lazima akatwe tsh. 8,340. Hivyo fedha ya ziada ya makato mtu anapaswa kuongeza Tsh 12,480 ili mama yake apate fedha kamili tsh. 200,000. Kabla ya tozo hii ya Serikali mtumaji angepaswa ongeza tsh. 6500 tuu ili mama apate fedha kamili tsh. 200,000.

Kwani serikali ingekosa nini katika muamala wa laki mbili ikakata elf moja tuu na akatwe anayetoa, serikali ingekosa nini?

Leo hii laki mbili anakatwa 2940, akituma anakatwa hiyo akitoa anakatwa hiyo.
Kwani angekatwa buku tu serikali ingekosa nini?

Kanuni ya makusanyo ya kikodi yanasema unavyotoza makato makubwa zaidi , ndivyo unapunguza wigo wa walipaji , ila unavyotoza kiwango kidogo na kwa unafuu unapata wigo wa mkubwa wa walipaji sababu ya kuwa na uwezo wa kulipa ("The ability to pay principle"). Tozo hizi za serikali ni kubwa mno na zinapunguza mzunguko mkubwa (Flow) ya miamala sababu watu wengi hawatakuwa na uwezo wa kulipa (Ability to pay principle) hivyo kutotumia miamala ya simu.

Serikali ingeweza kukusanya zaidi kwa kutoza kiwango kidogo na kwa muamala wa upande mmoja tuu,kwa sababu hii,mizunguko (flow) ya miamala ingekuwa mikubwa zaidi watu wangeendelea kulipa bila maumivu na serikali ingepata zaidi kwa kutoza kiwango kidogo kwa walipaji wengi kuliko sasa Serikali inatoza kiwango kikubwa, matokeo yake mizunguko ya miamala itashuka na serikali hatimaye itapata kidogo zaidi. Hata huyo Mh.Zungu alishauri kukata tozo ya sh.50 hadi 100, hakushauri kiwango kikubwa namna hii.
 
Serikali ingeweza kukusanya zaidi kwa kutoza kiwango kidogo na kwa muamala wa upande mmoja tuu,kwa sababu hii,mizunguko (flow) ya miamala ingekuwa mikubwa zaidi watu wangeendelea kulipa bila maumivu na serikali ingepata zaidi kwa kutoza kiwango kidogo kwa walipaji wengi kuliko sasa Serikali inatoza kiwango kikubwa , matokeo yake mizunguko ya miamala itashuka na serikali hatimaye itapata kidogo zaidi.Hata huyo Mh.Zungu alishauri kukata tozo ya sh.50 hadi 100 ,hakushauri kiwango kikubwa namna hii.
Mwigulu hajawahi kuwa na akili, hizo GPA anazojivunia ni za makaratasi tena kukariri siyo reasoning, he will never understand this lesson hata ungemsimamia na bunduki.
 
Mh @mwigulunchemba hii hoja ya kwamba serikali imekusudia kuingiza au kuachia tsh.trilion tano kupitia kulipa wazabuni wanaoidai serikali ili ziingia katika mzunguko na kwa wananchi, hoja hii na kwa sasa kutokana na makato ya tozo hizi ni absolutely Zero-Sum Game...
Hujui chochote kuhusu maswala ya uchumi, funga domo tu
 
Ukitaka kujua kwamba Mwigulu alimeza slides wamesema kodi ya mshikamano inaenda kujenga madarasa na vituo vya afya hii ya kwake anayoinject kwenye Uchumi ameitoa wapi? Miradi gani ya Uchumi anainject fedha hizi hawa ni watu wajinga na wapumbavu sana.

IMG_20210718_094029.jpg
 
Mh @mwigulunchemba hii hoja ya kwamba serikali imekusudia kuingiza au kuachia tsh.trilion tano kupitia kulipa wazabuni wanaoidai serikali ili ziingia katika mzunguko na kwa wananchi, hoja hii na kwa sasa kutokana na makato ya tozo hizi ni absolutely Zero-Sum Game...
Serikali hauwezi kukubaliana na wazo la kutokuwa na pesa za miradi.

Hii nchi ni tajiri na huwezi kufaidika na utajiri kama hujaifungua nchi kwa njia mbalimbali za kimawasiliano, ndege na treni.

Ujerumani ina uchumi mkubwa lakini msingi wake ni uwepo wa miundo mbinu rafiki sana kwa mahitaji ya uzalishaji. Na Ulaya nzima inakua kiuchumi ikibebwa na urahisi wa mawasiliano.

Hatuwezi kuiona faida ya reli hivi leo lakini inakuja miaka mbeleni watanzania wataielewa.

Hatuwezi kuona faida za ndege hizi leo hii lakini miaka inakuja watu wataiona.

Kuna suala zima la kusomesha wanafunzi wa vyuo na kuna suala la kinamama wanaofia njiani kwa sababu ya miundo mbinu duni.

Kuongoza nchi ni kazi ngumu sana kuliko wengi wetu tunavyodhania.
 
Mwigulu yupo sahihi wew jamaa hujui uchumi vema
 
Ukitaka kujua kwamba Mwigulu alimeza slides wamesema kodi ya mshikamano inaenda kujenga madarasa na vituo vya afya hii ya kwake anayoinject kwenye Uchumi ameitoa wapi? Miradi gani ya Uchumi anainject fedha hizi hawa ni watu wajinga na wapumbavu sana.

View attachment 1857907
Hivi hizi ziko parking gani [emoji1787]

Nataka nikazitembelee[emoji1787]
 
Wanasubiri wakusanye trilioni 5 kutoka kwa wanyonge ili wawalipe matajiri wachache Hii yote ni kwa sababu hatuna tume huru ya uchaguzi
tume inaingiaje kwenye makusanyo ya kodi? kweli nyie mme changanyikiwa
 
Ccm imechoka na serikali yake......,,tatizo watengeneze wao wananchi wahenyeshwe kulipa magufuli alisema nchi inapesa yake yenyewe nyingi

Leo madeni gani tena
 
Back
Top Bottom