Hoja yangu kuhusu Lengai Ole Sabaya aliyekuwa DC wa Hai

Mfumo ndio ulimtuma aje The Don na club za Arusha atake wanawake wa bure?
Mbona bosi wake alihonga nyumba na ukuu wa wilaya?
Wanawake waliotekwa wajitokeze hadharani na kuhakikisha Sabaya anamaliza maisha jela. MeTooMovementTz kuhakikisha Sabaya anawajibishwa kwa maouvu aliyewatendea dada zetu.
 
Ni kawaida sana katika sheria, unabeba makosa na kutumikia adhabu kwa kuwa wewe ndio ulifanya kinyume na sheria, nafasi ya kujitetea kwamba ni mfumo haipo maana aliyetekeleza maelekezo ya mfumo ni mtu mmoja mmoja na atashtakiwa mmoja mmoja, na akikutwa na hatia atatumikia adhabu mmoja mmoja. Kwani hukumbuki akina Mramba walivyojitetea kuhusu maagizo waliyopata kwa Ben? Mbona mwisho wa siku wao ndio waliotumikia kifungo huku Ben akiwa huru anatunga kitabu chake?
 
1. Mitandao mechafuka,
Watu wanalalamika,
Machozi yanawatoka,
Sabaya wamemchoka,

2. Kila mtu ni Sabaya,
Wamsema kwa mabaya,
Sabaya kawa Sabaya,
Sabaya wamemchoka.

3. Mara wale kawaonea,
Hawa nao katufanyia,
Huyu nae namchukia,
Sabaya wamemchoka.

4. Sabaya hakamatiki,
Sabaya haonyeki,
Sabaya Hashauriki,
Sabaya wamemchoka.

5. Nilimsikia Mgwira,
Akimwonya kwa busara,
Sabaya akafura,
Sabaya wamemchoka.

6. Hivi kwanini Sabaya,
Kila mtu Sabaya,
Sabaya huoni haya?
Jina lako tumechoka.

7. Mitandao inasema,
Wewe mwingi wa dhuluma,
Unapokonya ndarama,
Jina lako tumechoka.

8. Cheo chako watumia,
Watu wako kubutua,
Watu unawaonea,
Jina lako tumechoka.

9. Nchi yetu ya amani,
Wainajisi kwanini?
Kwani wewe una nini?
Jina lako tumechoka.

10. Umekuwa mungu mtu,
Wajiona kila kitu,
Roho mbaya ina kutu,
Jina lako tumechoka.
 
Tuwaache hata watakaothibitika kuua na kuteka kwa sababu lilikuwa ni tatizo la kimfumo?
 
Sabaya apelekewe mahakamani haraka sana na DPP hata bila uchunguzi kukamilika.

Usishangae 2025 Sabaya akawa anasafishwa hadharani na Chadema kama walivyofanya kwa Lowasa

Na hapo ndio utajua fisadi mchafu ni nani kati ya huyo sabaya na chadema🤣🤣🤣🤣
 
Huyo jamaa kama hakukati sijui, ulichofanya umeleta tu ya chumbani hapa hadharani
 
Sasa kama ume sema ni tuhuma iyo pole una mpa yann ? Kwan kapatwa na msiba ?
 
Huna akili kabisa kitendo cha kuwaibia wafanyabiashara kwa kuwalazimisha wampe hela hilo tu linatosha sana kumuondoa
 
Elius umelipwa ngapi ? Kama Clouds wametumika kumsafisha ....kumbe ndio ameharibu sasa ajibu tuhuma
 
Utopolo mtupu
 
Kwayo alitenda makosa kwa sababu kulikuwapo support kutoka kwa mwajiri wake, Je mbona haya madudu hayakutokea mahali pengine? Kwanini yeye Sabaya ahusishwe na uharibifu wa mali za raia na sio wakuu wengine wa Wilaya?
 
Naomba unijibu haya maswali kwa ufasaha kama hutanijibu basi wewe ni mmoja wa wanufaika na uhuni wa sabaya
1[emoji186].kuchoma gari na kuharibu snake park za mwekezaji mzawa ilikuwa kazi aliyotumwa kufanya hai?
2[emoji186]. kuvamia hotel na kutaka kupewa kiasi cha fedha mara kadhaa hiyo ndiyo uenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wa wilaya aliyokuwa akihudumu?
3[emoji186].mashamba ya green house aliyoharibu kwa mwekezaji mzawa ukiwa kama mtetezi wake je unajua gharama za uwekezaji wake zaidi ya ekari kumi?
4[emoji186].tabia yakutembea na wake za watu kushika makalio wake za watu mbele ya waume zao hii tabia ndiyo aliyofundiswa na waliomzaa au ni hiyo mamlaka unayoitetea wewe?
5[emoji186].unatoka wilaya iliyoko kikazi anakuja mkoa mwingine wa arusha kuja kufanya uhalifu wakupora wafanyabiasha fedha na kuondoka hii imekaaje kiutawala ukizingatia yule alikuwa ni Dc?
NB- acheni chuki ,ubinafsi ,wivu ,uzandiki udwazi, ushwegedego, upumbavu na ukanda na mambo kadhaa wa kadha yanayofanana na haya ila bado ninanyongi pakuimwagia sina mwana walegeza.
 
Naomba nikuulize swali Mkuu; Hivi viongozi kama Mkuu wa Mkoa wa Simiyu na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma (sehemu ambapo watu wote maarufu wanafikua na kukaa), mbona hatukusikia wakifanya ujinga na uhalifu wa akina Makonda, Hapi, Sabaya na Jerry Muro?
 
Kama kweli hii Basi ni hatari kubwa!
 
Naomba niulize jamani, huyu jamaa anazungumzia mfumo gani ambao ulimfanya huyu jamaa kutenda mambo ya ovyo akiwa kwenye ofisi ya umma?
Alifanya nini mkuu mbona hizo ni kalele tu za watu wa mtandaoni
 
Licha ya mfumo wa mwendazake kuonekana kuruhusu udhalimu. Wako wakuu wa wilaya wengi wakuikuwa waadilifu. Sabaya alifanya yote huku akiijua sheria na kuacha kwa makusudi kuitekeleza.
Kama huoni kosa la Sabaya wenye ufahamu ulioukosa watatilia shaka utimamu wako.

Sent from my SM-A705FN using JamiiForums mobile app
 


11. Sebaya mdudu baya
Baradhuli aso haya
Akilize ka malaya
Jina lako tumechoka.
 
Pole kwa msiba
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…