Hoja Yangu Leo: Lazima Timu ya Simba ifanye Usajili wa Golikipa

Hoja Yangu Leo: Lazima Timu ya Simba ifanye Usajili wa Golikipa

Mawembasa1979

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2015
Posts
2,540
Reaction score
3,333
Ni muda mrefu sasa mimi kama mpenzi na shabiki wa mpira wa miguu ambao ni mchezo namba 1 kupendwa sana duniani na Tanzania ikiwemo, nimekuwa nikifuatilia mechi mbalimbali za mpira wa miguu hapa nchini na duniani kwa ujumla. Hakuna ubishi, Timu ya Simba ina kikosi bora katika msimu huu ingawa kwa kiasi fulani kinawavunja moyo na nguvu wanachama, mashabiki na wapenzi wake (Simba Fans) kutokana na kucheza “kifarther” zaidi.

Nikijikita kwenye hoja yangu naomba leo tujadili kuhusu nafasi ya Golikipa katika Timu ya Simba. Binafsi, nimewaangalia Magolikipa wote watatu wa Simba Manula, Munishi na Salim. Bila ubishi katika hao watatu mwenye uwezo mkubwa ni Manula hasa kwa kuangalia takwimu (statitstics) ya aina ya mechi anazocheza ikilinganishwa na wenzake. Nimeuangalia udakaji wa Munishi ni kama vile hayupo sawa kisaikolojia. Maana anadaka mpira as if hayupo uwanjani. Hata anapokuwa amedaka mpira au ameukosa unamwona anasemasema peke yake (refer match ya Mashujaa FC). Huyu mwingine anaitwa Salim ndio hayuko fit kabisa kama mlimwona jana kwenye mechi na Chipukizi ya Pemba alikuwa anababaika sana. Kama usingekuwa uimara wa backline yake nadhani tungeyaona mengine jana.

Sasa basi, kwa muktadha huo unaona kuwa ikitokea iwe kwa bahati mbaya au nzuri Manula asiwepo langoni hali ya Timu ya Simba kimchezo itakuwa tete. Hasa kwenye kipindi hiki ambacho Simba inakabiliwa na Michuano Mikubwa na yenye manufaa kwa vilabu vya Afrika. Ikiwezekana Simba wafanye mazungumzo na Yanga ili wamuongeze Benno Kakolanya kwenye kikosi chao maana naona Yanga ni kama wamemtosa. Hasa katika michuano hii ya Champions League maana timu kwa kipindi fulani huruhusiwa kuongeza wachezaji watatu kama sikosei.

Tofauti na hayo Wana Simba mjiandae kisaikolojia ikiwa Manula hatakuwepo langoni.

Nakaribisha mjadala.
 
Nafikiri kuna haja ya uongozi pamoja na bench la ufund kuongea na kakolanya,tunahitaji kuwa na kikosi imara na kipana zaidi kuelekea mashindano ya klabu bingwa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wataongeza juhudi baada ya post hii, nani anataka kwenda ligi daraja la tatu?
 
Una hoja,hebu fikiria Manila akapata majeraha,huko Championship itakuwa aibu
 
Una hoja,hebu fikiria Manila akapata majeraha,huko Championship itakuwa aibu
Mimi mwenyewe ndio kilichonisukuma kuleta hoja hii kwenu mkuu. Binafsi ni mpenzi na mshabiki wa Yanga. Hata hivyo, Simba ni mwakilishi wa nchi hivyo ni muhimu kwetu sote kuweka mapenzi ya timu pembeni na kusaidia kuiwezesha Simba kufanya vizuri. Hii itakuwa ni promotion kwa nchi na faida kwa Timu zingine za Tanzania endapo Simba itafika hatua nzuri.
 
Back
Top Bottom