Naona hata hao makamishna wa katiba wana matatizo wanapashwa kutoa elimu kwanza kwa watz waelewe nchi hii haina dini tunachotaka ni maendeleo hata ikibidi tubadili majina yetu yawe ya kienyeji ili kuondoa huu udini unaotusambaratisha! Tutachinjana wenzetu watakuja kuvuna kiulaini.
Kwa hali tuliyonayo hata hizo siku za mapumziko zilitakiwa zisiwepo kwani tunatakiwa tujitume sana ktk nyanja zote ili kumkomboa mtanzania. Umasikinu utaondolewa kwa kila mtu kujituma katika fani zote na huo muda wa kupumzika siuoni. La msingi ili kutuliza akili mapumziko yanatakiwa kwa ratiba fulani siyo Ijumaa au Jumapili. madereva, madaktari na mawasiliano hawafuati ratiba hii. Mwabudu Mungu wako kwa wakati wako atakusikiliza tuu. Chapeni kazi wa tz porojo za nini. Mpaka nafikiria labda jeshi lingechukua madaraka.