KARLO MWILAPWA
JF-Expert Member
- Apr 10, 2019
- 2,789
- 4,951
Habari,
Kwa mawazo yangu, upinzani ni upande wenye fikra, sera, mawazo na maoni mbadala wa chama kilichopo madarakani. Hivyo basi, katika nchi nyingine watu hufikiri kwenda na upinzani kwa sababu ya sera mbadala ilizonazo katika uongozi.
Hali hii ni tofauti na hapa kwetu Tanzania, watu wanaona upinzani kama dodoki la kusafishia mafisadi, wala rushwa na wengineo na mifano katika hili ipo dhahiri kabisa. Hii inaleta hofu kwa watu kuuelewa upinzani una dhamira gani kwa nchi yetu?
Tukiachana na hilo la kuwa dodoki, upinzani umejijenga katika kujenga hoja dhaifu sana. Kwa mfano kuna mmoja alipoulizwa juu ya michango ya kampeni za Lissu akaishia kujibu kwamba tayari tumeichangia CCM kwenye kodi zetu.
Hii jibu ni mtu mwenye hoja dhaifu anaweza kujibu na kwa majibu haya ni dhahiri nia ya upinzani si njema kwa taifa letu ila tuendelee kuwasikiliza na kuwapima zaidi ili tusifanye makosa ya kuchagua.