Hoja za Warioba zijibiwe, zisipigwe Rungu!

Comrade sio kweli kuwa kila mwana CCM yupo namna hii! Jaji Warioba ni CCM, Mzee Butiku ni CCM, Dr. Hussein Mwinyi ni CCM, Dr. Nchimbi ni CCM n.k
Hawa wanashida gani?
 
Gentleman,
huyo mzee hajawahi kuamini anachosimamia, wala kujiamini hata alipokua waziri mkuu, waziri wa katiba na jaji mkuu wa Tanzania. Alikua ni muoga kupindukia na ndio maana hajaacha legacy yoyote zaidi ya kushindwa uchaguzi na Stephen Masatu Wasira katika jimbo la Bunda wakati huo.

hakua na msaada wowote kwa nchii hii. Alikua mfuata mkumbo bora liende tu.
Kutokupewa nafasi kwenye tume mbalimbali anazounda Rais, kumemfanya azidishe chuki na hasira dhidi ya serikali sikivu ya CCM na viongozi wake wa kitaifa.

Kiufupi,
mzee warioba ana tamaa sana ya vyeo lakini kiukweli kabisa hana uwezo kiutendaji, na ndio maana anayumbishwa na kila anaetaka kumtumia na kumpa nafasi ya kutweza heshima yake kwa uongo na uzushi mitandaoni na kwenye vyombo vya habari.

Kuhusu kumbishia Nyerere au Sokoine kwa lolote lile ni uongo wako mwenyewe, huenda unalenga kuwapiga kamba wasiomfahamu. Wahujumu uchumi katika kipindi cha nyere na sokoine waliwajibishwa ipasavyo yeye akiwa anatazama na kushangaa tu akiwa waziri wa katiba. Hakua na ubavu wa kumbishie yeyote wakati huo.

Anajojaribu kueleza, tayari kimeelezwa na tume ya jaji chande ila kwa ubinafsi wake anajaribu kujimilikisha kilichoelezwa na tume ya jaji chande kana kwamba yeye anaeleza kitu kipya.

Aache chuki dhidi ya kazi za majaji wenzake,
na lazima awe na adabu kwa sheria na katiba ya nchi pia.
 
Gentleman,
ikiwa umefikia kiwango chako cha mwisho cha fikra mpya na mawazo mbadala dhidi ya hoja mahususi mezani, unakaa kimya tu na itapendeza zaidi,
kumbwelambwela porojo na uzushi nonsense kama wa mzee warioba, ni vitu useless sana visivyo na athari zozote kisiasa Tanzania.

Nasisitiza kwamba mzee warioba apuuzwee,
na kama taifa tusonge mbele pamoja bila kuzingatia wala kutilia maanani upotoshaji na porojo za warioba mwenye chuki binafsi na ambae inaonyesha ni kama amechanganyikiwa hivi.
 
Usipoteze muda wako na huyu. Ni excreta ya watawala!
 
Hakuna mtu wa ccm ama serekali anaweza kujibu ukweli wa Warioba kwa hoja.
 
Huyu unayemjibu hapa ni aina ya wanaccm wengi kwa sasa,. Na kwa bahati mbaya baadhi ni viongozi na ndio waliomwagwa huku mitandaoni kujibu hoja. Sehemu kubwa sio wajibu hoja bali ni persanal attack. Hiki anachoongea huyu jamaa usishangae Mwigulu ama Kabudi akarudia hivi hivi hadi nukta.
 
YY mwenyewe warioba hajui anaongea nn hakupaswa kupewa airtime lakin kwasababu tuna waandishi wa habar wasio na maadili ndo maana wanaweza report hata habar za kichaa
Warioba anao uelewa mpana kuliko hata wewe na Samia katika nyanja za siasa za chama , kitaifa na kimataifa.

Hili pia linajidhihirisha kwa aina yako ya uandishi ndio bado unataka kujilinganisha na Warioba wewe mwalimu.?

Uandishi wa kuandika "YY" , "nn", " lakin", "habar" , "ndo" unanipa wasiwasi hata hao wanafunzi unaowafundisha wana hali gani kitaaluma?

Nakukumbusha tena wakati Samia anapata daraja 0 kidato cha nne mwaka 1977 , Warioba nafasi yake alikua mwanasheria mkuu wa serikali.
 
Comrade unatuonea, hatujachoka kiasi hicho.
Ukweli usemwe , kabla ya 1992 kila mtanzania alilazimishwa kuingia CCM baada ya watu kutoka CCM walienda kutumia akili zao vyema japo hawakukosekana matapeli wa kisiasa ila kwa sasa CCM imeishiwa "think tanks"

Jaribu kupitia katika mijadala mitandao ya kijamii uone ulinganifu wa vijana wa CCM na vijana wa CHADEMA na wale wasio na upande wa vyama ila wanataka mabadiliko utajionea tofauti katika ujenzi wa hoja katika mijadala tunduizi.

Alaumiwe Magufuli aliyezuia siasa vyuoni ndio aliwaharibia vijana uwezo matokeo yake wakakabidhi akili na kuzaliwa kitu kipya kiitwacho uchawa.

Ni mwaka juzi tu Nchimbi aliingia mitini katika mdahalo wa makatibu wakuu wa vyama hiyo ikupe picha CCM ilivyochoka.

Na kwa kuthibitisha hilo nieleze ni mwaka gani mara ya mwisho CCM na viongozi wake wamefanya mdahalo wa wazi .
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…