Ukisema Wayahudi ni wavamizi, unaonekana ni mjinga, usiyeijua historia. Ukweli ni kuwa nchi ya Canaan, kiuhalisia ilikuwa ni ardhi ya makabila yale 12 ya Israel lakini wakati wote kulikuwepo na jamii nyingine kwa idadi ndogo kwenye eneo hilo hilo..
Kutokana na vita mbalimbali, na kwa kuzingatia hiyo jamii ya Wayahudi ilikuwa imepata mandeleo ya kiasi fulani kuyazidi makabila mengi, waliweza kusafiri na kuishi katika mataifa mbalimbali, na hivyo kuiacha sehemu kubwa ya ardhi ya Baba zao, na hivyo kutoa nafasi kwa vizazi vya Waarabu kujichukulia ardhi hiyo na kuifanya kuwa ya kwao pekee yao. Uharamia wa Hitler dhidi ya Wayahudi, kuliwafanya Wayahudi kuikumbuka nchi ya baba zao, na hivyo chini ya kampeni ya Zionism, Wayahudi wote kokote waliko, walihamasishwa kurudi ilikokuwa nchi ya Canaan. Waliporudi, sehemu kubwa ya nchi hiyo iliyokuwa ya Canaan ilikuwa imechukuliwa na Misri, Lebanon, Syria na Iraq. Wayahudi walikuwa tayari kuishi pamoja na wale Waarabu waliowakuta kwenye ardhi ya Baba zao, eneo la Palestine, lakini kwa ushawishi wa nchi za Kiarabu, Waarabu wa Palestine, walikataa kuwa sehemu ya nchi ya waliyotaka itambulike kwa jina la Israel. Waarabu wa Palestine wakagawiwa 40% ya eneo lote, nchi za kiarabu zikawashawishi waarabu wa Palestine kuwa wasiikubali hiyo 40% maana wao Waarabu watawasaidia kuwaua Wayahudi wote ili wao waarabu wa Palestine walichukue eneo lote, matokeo yake, mambo yakawa kinyume. Waarabu wa Palestine wakazidi kupoteza ile 40%, na leo wamebanana kwenye eneo lisilozidi 10%.
Nchi za Kiarabu, hasa Misri, Iran, Syria, na Lebanon ndiyo za kulaumiwa katika kuwafanya waarabu wa Palestine kukosa kuwa na ardhi, na hata kuendelea kwa hivi vita vinavyoangamiza maelfu ya watu wasio na hatia.
Suluhisho lipo, lakini kwa sasa, kikwazo kikubwa ni Iran.