SoC03 Homa chini ya 18 na juu yake: Kliniki endelevu

SoC03 Homa chini ya 18 na juu yake: Kliniki endelevu

Stories of Change - 2023 Competition

Mamshungulii

Senior Member
Joined
May 3, 2023
Posts
175
Reaction score
88
HOMA CHINI YA 18 NA JUU YAKE : KLINIKI ENDELEVU

Kwa mujibu wa Tamko la Umoja wa Mataifa (1989) na kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (1977), Mtoto ni mtu yeyote mwenye umri chini ya miaka 18.

Katika uchokoraa wangu uliopo damuni ndipo hujikuta nasoma ,magazeti ,na mitandao mengine mingi ya kijamii kupitia ka simu kangu ka tekno ndipo nikapata taarifa katika gazeti la Nipashe la Disemba 14,2022 toleo namba 0581159.

Mwandishi alimnukuu Mratibu wa Mpango Kazi wa Taifa wa kutokomeza ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto (MTAKUWWA) akitaja kwamba, mwaka kati yaa Januari hadi septemba 2022 kulikuwa na matukio shambulio la kudhuru mwili 3,322,ulawiti 1,044,mimba kwa wanafunzi 1,115, lugha ya matusi 1,858,kushambulia Watoto 3,100,kujeruhi Watoto 2,141.Kisha alitoa wito Pamoja na mambo mengine kuendelea kutoa elimu ya malezi ya Watoto.

Kwa ninayoyaona hapa Mwanza mjini nimeona umuhimu na ulazima wa kuthubutu kuchukua hatua ya kuandika Makala hii ili kuielimisha,kuikumbusha ,kuihimiza na kuhamasisha jamii juu ya haki,ulinzi,usalama na malezi/makuzi yetu ya Watoto.

Hali ilivyo sasa ni mbaya Watoto wengi wanapitia mateso makubwa sana ya ukatili na unyanyasaji wa namna mbalimbali unaofanywa na watu wazima au baina ya Watoto wenyewe kwa wenyewe.Simulizi za visa vingi vya dhulma kwa Watoto zinadhihirisha wazi kwamba,kuna changamoto ya uelewa mpana wa wazazi ,walezi na jamii kwa ujumla kuhusu haki na usalama wa Watoto.
Mathalani,ni wazazi,walezi,Watoto wenyewe au wanajamii wangapi wajuao kwamba kwa mujibu wa Sheria ya mtoto Na .21 ya mwaka 2009.

…kila mtoto ana haki ya kulelewa na wazazi,haki ya kupewa jina na utaifa,haki ya kupata mahitaji ya msingi kama chakula ,malazi,mavazi,matibabu,chanjo,elimu,Pamoja na haki ya kucheza na kuburudika .
Pia…watoto wana ruhusa ya kufanya kazi baada ya kutimiza umri wa miaka 14. kazi haipaswi kumzuia mtoto kuhudhuria masomo au kupata muda wa kujisomea na kkupumzika.watoto wasiajiriwe kufanya kazi za usiku.Yeyote anayewafanyisha kazi Watoto kupita kiasi, au asiyewalipa ujira unaostahili,basi anavunja sheria hii!

Uvunjaji wa sheria ama kwa kujua Au kwa kutokujua husababisha vitendo vya ukatili kwa Watoto na matokeo yake ni Watoto kushindwa kufurahia kuwa Watoto.Kutokufurahia utoto wao,kunaleta madhara makubwa ya kisaikolojia,kiakili,kimwili.Kwasababu ,mtoto ambaye ni mwathirikka wa ukatili huwa anawaza ukatili anaotendewa kuliko kuwaza mambo ya kawaida ya utotoni kamavile masomo,michezo na marafiki.

Maandishi haya ni kama alamu ya saa kutukumbusha na kutuhimiza sote na hususani serikali kuchukua hatua za makusudi za kuendelea kutafuta kiini halisi cha kushamiri kwa vitendo vya ukatili dhidi ya Watoto kila uchwao. Aidha,Serikali na wadau wengine wote waone umuhimu na ulazima wa kuendelea kuelimisha umma kuhusu Sera,Sheria na kanuni za masuala ya haki za Watoto ili kupunguza na hata kuondoa kabisa tatizo hili.

Ni muhimu kuzingatia kwamba ,utafiti umethibitisha kuwa Watoto wanaopitia dhuluma Fulani katika utoto wao.Huwa na uwezekano mkubwa zaidi na wao wenyewe kuwadhulumu Watoto wao au wenzi wao au watu wengine au pia kudhulumiwa tena katika utu uzima wao.
Ulinzi wa mtoto ni hali ya kumlinda mtoto dhidi ya vitendo vya ukatili na kumtunza ili awe salama.

HAKI YA WATOTO
Haki ya Watoto ni vifungu vya haki za binadamu,haya ni makubaliano ya wanachama wa umoja wa mataifa yanayozungumzia mtoto ni mtu mwenye umri chini ya miaka 18 hivyo ana haki ya kulindwa Pamoja na haki nyinginezo za msingi.

Mtoto ana Haki ya….
1. kupata elimu bora,
2. kulindwa
3. kupata lishe bora
4. kucheza
5. kulelewa na wazazi wote wawili
6. huduma za afya
7. kuoneshwa upendo kuambiwa ninakupenda…na kuonywa pia….
8. kupewa jina
9. Kusikilizwa, kushirikishwa na kutoa maoni yake

MAJUKUMU YA MTOTO
a) Heshima kwa wazazi Pamoja na watu waliomzidi umri
b) Kufanya kazi kwa bidii
c) Kushirikishwa au kushiriki kazi ndogondogo za nyumbani au shuleni
d) Kujiepusha dhidi ya tabia na vitendo hatarishi
e) Kusoma kwa bidii
f) Kuhudhuria ibada

MAHITAJI MUHIMU KWA UKUAJI WA MTOTO
• AFYA,
• LISHE,
• ULINZI,
• UPENDO,
• ELIMU,
• IBADA.

AJIRA ZA WATOTO:
Ajira kwa Watoto kunaweka mtoto katika hatari ya kupata madhara ya moja kwa moja au yasiyo ya moja kwa moja ,yafuatayo:-
i. Kulipwa mshahara chini ya kiwango
ii. Kufanya kazi chini ya kiwango
iii. Kipigo na matusi
iv. Kubakwa kwa kunajisiwa au hata kulawitiwa
v. Kulazimishwa kufanya kazi hatarishi na zisizo zake.
vi. Kutokupewa muda wa kupumzika
vii. Kudhulumiwa haki yake ya kuwa mtoto
viii. Kulazimishwa kukua kabla ya umri wake
ix. Kujifunza tabia na vitendo viovu kama vile kuvuta sigara,kunywa pombe, lugha ya matusi,kukosa huruma.
x. Kuwa mzazi katika umri mdogo
xi. Kupata mimba katika umri mdogo

MALEZI YA MTOTO
Malezi ni mchakato wa maandalizi ya mtoto utakaomwezesha kukua,kukubalika na kushiriki katika shughuli za kijamii na kiutamaduni kwa kumlinda ili kupata mahitaji na huduma
CHANGAMOTO ZINAZOMKUMBA MTOTO
a) Ujinga wa wazazi juu ya malezi bora kwa Watoto
b) Umasikini katika familia
c) Kuachana kwa wazazi
d) Kuzaa bila mpangilio
e) Ugomvi mbele ya watoto

NINI KIFANYIKE KUMUOKOA MTOTO?
1. Watoto wote wanaozaliwa Tanzania na ambao wapo katika umri wa kusoma msingi na sekondari wawe na kadi endelevu maalumu za utambulisho, kadi hizo ziwe za kielektroniki ili kurahisisha usalama wao na uwajibikaji wao kama watoto na katika hizo kadi zionyeshe grupu la damu ili hata endapo ajali au mtoto akipungukiwa damu popote iwe rahisi kuongezewa...

2. Watoto wa mashule wasajiliwe majina na picha zao kielektroniki hata endapo mtoto akipotea au asipohudhuria shuleni iwe rahisi kwa watu wenye dhamana kufuatilia kwa haraka. Kabla ya mtoto hajadhurika au kupostiwa kwenye mitandao ya kijamii.

3. Kadi hizo za watoto ziwe maandalizi ya kadi za nida kufikia umri wa utu uzima kikatiba, kwamba mtoto atapaswa atoe gharama kubwa zaidi kama hana kadi ya utoto afikishapo umri wa miaka 18 na kuendelea.

4. Nzengo zinao utaratibu mzuri wa kuwawajibisha watu washiriki katika misiba na harusi au hata mikutano ya kisiasa lakini nzengo hizohizo hazitilii mkazo kuweka utaratibu mzuri kuhakikisha malezi ya watoto yanatiliwa mkazo.

5. Taasisi binafsi hazishirikiani katika kuhakikisha zinawaondoa watoto kupelekea mtoto mmoja akiwepo mtaani kudanganya na kuhudumiwa na taasisi zaidi ya moja na kuchochea kuufanya uchokoraa kama mtaji usiokuwa na manufaa.

6. Watoto wa mitaani imekuwa kama mtaji kwa baadhi ya watu kujiingizia pesa hivyo watu wa hivyo wakibainika wawajibishwe .

7. Kuyavunja magenge ya watoto ambao wameathiriwa na mtaani.
 
Upvote 2
Back
Top Bottom