Herbalist Dr MziziMkavu
JF-Expert Member
- Feb 3, 2009
- 42,872
- 34,363
Homa ya Nyani: Kwa nini Mpox inaenea kwa kasi Afrika Mashariki na Kati?
Maelezo ya picha,Homa ya Nyani ilianza kwa wanyama kwenda kwa binadamu huko Afrika ya Kati na Magharibi, sasa inaenea kupitia wanadamu.Maelezo kuhusu taarifa
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), imekumbwa na ongezeko la wagonjwa wa homa ya nyani ama Mpox. Hilo limepelekea hatua za dharura za afya kwa umma kuchukuliwa.
Uganda pia imethibitisha kesi mbili mpya za Mpox, kama ilivyo kwa Kenya, Rwanda na Burundi katika ripoti kuhusu milipuko wa homa hiyo Afrika Mashariki.
Kwa mujibu wa ripoti ya Africa CDC, idadi ya kesi zimeongezeka ikilinganishwa na mwaka jana, na idadi ya vifo imeongezeka vilevile.
Umoja wa Afrika umeidhinisha dola milioni 10.4 kutoka katika fedha zilizopo za Covid kusaidia Afrika CDC, katika kukabiliana na mlipuko wa Mpox katika bara zima.
Kesi nyingi na vifo viko katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Mwaka huu pekee, kumekuwa na visa zaidi ya 8000 vilivyoripotiwa na zaidi ya vifo 300.
Dk Fiona Braka, Meneja wa Dharura wa Shirika la Afya Duniani nchini Congo Brazzaville, anasema "kesi zimeripotiwa katika nchi 11 za eneo hilo tangu mwanzoni mwa 2024."
"Tunaona kesi nyingi zaidi nchini DRC, ambayo inachukua asilimia 96 ya kesi zote ambazo zimeripotiwa katika eneo hili," anasema.
Visa viwili vya ugonjwa huo unaoambukiza viliripotiwa hivi karibuni nchini Rwanda na Jamhuri ya Afrika ya Kati, (CAR), siku chache tu baada ya Burundi kutangaza uthibitisho wa kesi.
Hivi karibuni, nchi jirani ya Kenya pia imeripoti kisa kilichogunduliwa kwa msafiri aliyekuwa akitoka Uganda kwenda Rwanda kupitia kivuko cha mpaka kusini mwa nchi hiyo.
Hali hii imezua wasiwasi kuhusu kuenea kwa aina mpya na mbaya ya ugonjwa huo.
Afrika Kusini pia ilirekodi visa vya virusi hivyo, na vifo vitatu, lakini vipimo vya awali vinaonyesha maambukizi hayo yamesababishwa na aina isiyo hatari sana ya virusi hivyo.
Wataalamu wa afya wanasema virusi hivyo vinabadilisha tabia yake, vinajitokeza miongoni mwa makundi mapya, kama vile wafanyabiashara ya ngono.
Ugonjwa huu huenea kwa njia ya mawasiliano ya kimwili na ya ngono na unaweza usigundulike kwa kutazama kwani baadhi ya watu hawaonyeshi dalili. chanzo.BBC