Sildenafil Citrate
JF-Expert Member
- Jan 29, 2021
- 577
- 2,595
Shirika la Afya Duniani (WHO) leo Mei 11, 2023 limetangaza rasmi kuwa Ugonjwa wa Homa ya Nyani (Mpox) sio tena janga la Dharura ya Kimataifa.
Taarifa hii inakuja siku moja baada ya kamati ya Dharura ya ugonjwa huo kuketi na kutoa tathimini kuwa kwa sasa ugonjwa huo haustahili tena kuwa dharura ya dunia.
Shirika hilo liliutangaza ugonjwa wa Homa ya Nyani mwezi July, 2022 kuwa dharura ya dunia baada ya kutokea milipuko kadhaa iliyotishia usalama wa dunia.
Hadi sasa jumla ya nchi 111 zimethibitisha kuathirika na ugonjwa huu, visa 87,000 vimeripotiwa na vifo vikiwa ni 140.