Home tips

rubii

JF-Expert Member
Joined
Feb 22, 2015
Posts
14,032
Reaction score
18,540
Wakuu njooni, kuna mtu hapendi kuishi nyumba safi nzuri na salama?

Nyumba ni nyumba hata iwe chumba cha kupanga. Binafsi huwa naandaa home tips zinazogusa nje na ndani ya nyumba, sittingroom, kitchen area, Washrooms/Maliwato, bedroom. Basi karibuni nitakuwa naziweka hapa pia kama unayo unaweza kushare tukajifunza wote.

Nawezaje kufanya chumba kidogo kionekane kikubwa?

1. Paint and Color
Dark na bright light colours hufanya chumba kionekane kikubwa zaidi.
Ukihitaji wallpaper, tumia horizontal stripes kufanya kuta zionekane ndefu kwenda nani zaidi na vertical stripes kufanya zionekane ndefu kwenda juu.

2.Furniture
Usiweke zikagusa ukutani kabisa acha nafasi kati ya ukuta na furniture zako kwa zile fupi eg: sofa sets
Kwa furniture ndefu ziweke kuegemea ukuta. πŸ€” makabati

3. Lighting
Natural light inahitajika sana kukuza muonekano wa room yako basi weka pazia zenye rangi neutral ama nyepesi kuruhusu mwanga zaidi.

Unaweza ongeza taa ndani ya chumba usitege mwangaza kutoka chanzo kimoja pekee. Tumia bedsidelamps Floorlamps ama wall lamps [zipo #dollrubiidecors].

4. Mirrors
Ongeza vioo kwa kuta zako.

5. Decorations and Artwork
Matumizi sahihi ya decorations za ndani huweza kusaidia kukuza muonekano wa nyumba yako. Go with one big art work kwenye ukuta wako na inatosha kuliko kuweka vipicha vingi vingi.

6. Reduce Clutter
Punguza vitu visivyokua na matumizi katika uso wako. Sio uvitupe la! Tafuta njia sahihi ya kuvitunza mfano Decor Baskets, Decor Boxes, Storage bench. Huko unaweza tunza vitabu, magazeti, pillows, blankets.


 
Safi sana.
 
Dah...safi sana....nimeipenda hii....ila kidogo umenichanganya kwenye dark and bright colours....pamoja na natural light....ndiyo zipi mkuu?
 
Dah...safi sana....nimeipenda hii....ila kidogo umenichanganya kwenye dark and bright colours....pamoja na natural light....ndiyo zipi mkuu?
Hellow darling natural light nimemaanisha mwanga halisi wa jua
Dark and bright colours ni zile waswahili huita rangi ngumu lakini zinawaka mfano dark green

Quote
 
Nyumba ni kitu muhimu na gharama ambacho kila mtu hulazimika kuwa nacho.
Nyumbani ni sehemu inatakiwa iwe utulivu, amani na salama
Hapa siongelei watu bali mpangilio wa nyumba husika.
Hizi ni dondoo chache kufanya uwe na nyumba tulivu na salama kwa matumizi ya kibinadamu kila siku.

1.Vua viatu vyako ukiwa mlangoni.
Soli za viatu vyetu zibaweza kubeba chemicals, bacteria na uchafu kutoka nje ambavyo havitakiwi kuingia ndani ya nyumba zetu.
Tope??? Mafuta? Kinyesi cha wanyama?
Embu kumbuka enzi za corona 🀨
Kama huna tabia hii basi Anza leo.
Usiingize viatu ndani bila kusafisha vumbi na taka nyingine
Hakikisha viatu vyako vinakaa katika mpangilio maalum vikiwa ndani


2.Punguza vitu visivyohitajika tena mara kwa mara.
Tumekua na tabia ya kutunza kila kitu ndani hata vile tusivyokua na matumizi navyo tena lakini kuwa na vitu vichache ndani inasaidia urahisi wa kufanya usafi,
Kuzuia mazalia ya wadudu...Ng'e, tandu mende mbu nk
Je vitu vya thamani nisivyotumia nivitupe😬??
[ ] Hapana, unaweza kuviuza kwa watu kulikoni vikae hadi kuharibika.
[ ] Unaweza kugawa kwa ndugu ama wale wenye uhitaji
[ ] Kama unaweza kuunda kitu kingine kupitia kitu hicho fanya hivyo.

3.Fanya Usafi katika kila kona iliyojificha na uvungu
Yes Si lazima kila siku lakini
πŸ˜ƒNani ataona??
Huwenda hakuna atakayeona lakini Afya yako ni jukumu lako .
Mara 1 kila wiki yafaa sana
Mazoea hujenga tabia.


4. ONdoa vumbi mara kwa mara.
Unahitaji hewa nyepesi na fresh ndani ya nyumba yako
Je huwa unafuta vumbi sehemu hizi??
Kitanda na juu ya furniture zote
Usisahau juu ya kabati Nyuma yake je πŸ₯±
Ukuta wako mara ya mwisho umesafishwa lini
Carpet lako?πŸ€”
Ndani la kabati???? Ukitoa glass hadi uzioshe 😜
Unaweza kutumia Airfresher au diffuser kuleta harufu ya tofauti ya kuvutia.
[ Nitaleta tips za kuvuia vumbi ndani]


5. ZIba matundu/nyufa zote na mashimo ndani na nje ya nyumba yako kwa kufanya hivi utapunguza makazi ya wadudu nyumbani kwako.

Kwa dondoo za nyumba zetu
HOMETIPS KILA SIKU
WHATSAPP πŸ‘‰πŸΎ0657185081
INSTAGRAM πŸ‘‰πŸΎdollrubii_decors
 
Kwahiyo ina maana chumba cha mita mbili unaweza kukifanya kikaonekana ni cha mita 5 kwa 5 ama mimi mnyiramba sijaelewa [emoji276]?
 
Kwahiyo ina maana chumba cha mita mbili unaweza kukifanya kikaonekana ni cha mita 5 kwa 5 ama mimi mnyiramba sijaelewa [emoji276]?
NI unyiramba wako tu mkuu
 
Hellow darling natural light nimemaanisha mwanga halisi wa jua
Dark and bright colours ni zile waswahili huita rangi ngumu lakini zinawaka mfano dark green

Quote
Dah....umenipatia sana darling πŸ₯°
 
Hapo kwenye vumbi ni kipengele, uje utupe tip za kusafisha vumbi kwenye frem za madirisha ya aluminium
Sawa rafiki niko nafanyia kazi hilo. Asante
 
Hivi ni baadhi ya vifaa vya usafi, kufanya usafi bila vifaa muhimu, huo sio usafi, na ndio mwanzo wa uvivu wa kutogusa sehemu zote za usafi.

Kuwa na vifaa vifuatavyo na hivi ni general vifaa:
β€’ Ndoo ya usafi na dekio na hii iwe ni kwa matumizi ya usafi tuuu, ama kuna wengine huwa wanatumia mop pia ni nzuri tuu inategemea na uwezo wako.
β€’ Fagio
β€’ Kizoleo cha taka
β€’ Dasta ziwe mbili ya kufutia vumbi, iwe mbichi na ingine kavu kwa ajili ya kukausha na ziwe ni cotton.
β€’ Brush, ama hoover kwa wale wenye carpets.
β€’ Ngazi ya kupandia (ikiwa ni lazima)
β€’ Fagio la kutoa buibui. etc
β€’ Taulo za karatasi [tishu]
β€’ Brashi ya choo
β€’ Brush ndogo za mkono

BIDHAA ZA USAFI
β€’ Glass cleaner kama unamiliki surface yoyote ya kioo hii ni must have
β€’ Bidhaa ya kusafishia zulia (ikiwa ni lazima)
β€’ Bidhaa ya kusafishia sakafu tumezoea sabuni za maji na zile za unga zote ni sawa
β€’ King'arisha samani/mbao
β€’ Bidhaa ya kusafishia oveni (jikoni tu)
β€’ Dawa ya kuondoa grisi (jikoni tu)
β€’ AIRFRESHER/DIFFUSER

Ukiwa na hivi vyote nakuhakikishia utakusa kila kona ya nyumba yako kwenye usafi. Na hakikisha vitu ambavyo huvitumii tupa ama gawa. ACHA KUJAZA MAVITU USIYOTUMIA NI MOJA YA UCHAFU HUOOOOOO!!!!πŸ’ƒπŸ»πŸ’ƒπŸ»πŸ’ƒπŸ»

Imeandaliwa na DollRubii

Kwa dondoo za nyumba zetu
HOMETIPS KILA SIKU
INSTAGRAM @dollrubii_decors
Kwa mahitaji ya Furnitures, Home decors Appliances na kitchen utensils




 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…