Homosexual ni mtu ambae mrengo wake wa kufanya mapenzi ni ya jinsia aliyo nayo. Kama yeye ni mwanaume basi yeye hupenda kufanya mapenzi na mwanaume mwenzake, hali kadhalika akiwa mwanamke naye ni hivyo hivyo. Hapo nyuma kidogo homosexuality ilikuwa kwenye moja ya magonjwa ya akili. Lakini kutokana na "wavumbuzi" wa Amerika, waligundua kuwa unaweza ukawa una vinasaba vinavyochochea mtu akawa anatamani kimapenzi wenzake wa jinsia moja. Hiyo ilisababisha kutolewa kwa huo "ugonjwa" kwenye daftari la magonjwa ya akili. Katika jamii tofauti homosexuals wanapokelewa kwa tabu kidogo. Nchi za magharibi wao wanaweza kuwavumilia mpaka sasa hivi wameruhusu ndoa za jinsia moja, kitu ambacho kimeleta tafrani na mizozo katika jamii zao. Nikirudi kwenye hoja yako kuwa huo ni mchakato tu unaweza ukabadilika hapo sikubaliani nawe. Mara mtoto wa kiume akianza kale kamchezo ka kupakuliwa 713 inakuwa ngumu sana kuacha.