Honda Accord: Shujaa aliesahaurika

Mad Max

JF-Expert Member
Joined
Oct 21, 2010
Posts
26,961
Reaction score
77,890
Kibongo bongo, Toyota hana mpinzani kwa idadi ya magari na "kuaminiwa" na watu. Ila sasa kwa gari "imara" used kutoka Japan, Toyota brand ndio inaweza kuongoza, ikifuatiwa na Honda namba tatu wacha wagombanie wakina Nissan, Suzuki na Subaru.

Sasa kwa upande wa best selling sedans kuna bwana anaitwa Toyota Camry na Corolla ila kwa Honda kuna Accord na Civic. Hatusemi wengine hawauzi ila wanauza ata zaidi ya hao ila sio worldwide, mfano Crown ilikua haiuzwi Marekani hadi ilipokuja hii Model ya 2023.

Sasa bwana sijui wapenzi wa Sedans wanafeli wapi, nimekutana na Accord chache sana hapa Dar. Kama 4 hivi ingawa najua zinaweza kua zaidi. Na nyingi ni generation ya 7 (2002) na ya 8 (2008).

Uzuri wa Honda Accord ina generations nyingi zaidi ya 11 kwahiyo imepitia maboresho mengi sana.

Imagine kitu kama hiki hapa utaamini kwamba ni cha mwaka 2013?


Sema ndio hivo imekosa wadau na ata ukiingia kwenye website maarufu za kuagiza magari unakuta zipo chache sana.

Kama wewe ni mdau wa Sedans, ebu cheki na Accord ni moja ya best car kwa sekta za reliability na fuel efficiency.
 
Hata Japan kwenyewe kampuni ya honda inashika nafasi ya pili Kwa mauzo na kuwa na magari yanayoaminika..
Ila honda Wana design mbaya ya magari Yao huwa siyaelewi Sana magari yao
 
Hata Japan kwenyewe kampuni ya honda inashika nafasi ya pili Kwa mauzo na kuwa na magari yanayoaminika..
Ila honda Wana design mbaya ya magari Yao huwa siyaelewi Sana magari yao
Hahahaaa

Siku hizi wameboresha. Sema bei ndio challenge. Mfano Honda Insight, Civic, Vezel, Fit, Accord za miaka ya 2016 kuja juu 🙌🙌
 
Changamoto ya Honda ni spear. Spear zake ni shida kubwa.
 
Tatizo ni calculator ya TRA
Sijui uwa wanatumia vigezo gani katika kupanga (sio ku calculate) izi gharama zao.

Ona mfano hapa tuna Honda Accord ya mwaka 2014 ushuru:

Hafu chini yake tuweke BMW ya mwaka huo huo 2014 ushuru:

Yaani BMW ina ushuru chini ya Honda kwa Million 4.5 hivi. Why?

Ukisema bei nakukataa. Kwasababu BMW inavotoka mwaka 2014 iliuzwa above $32,000 wakati Honda Accord ilianzia $22,000.

 
Ukosefu wa taarifa unaweza kuwa sababu ila kwa uchumi wa wabongo hizo bei anaona bora ajichukulie magari ya biashara awe transporter..

Bei ya accord used kulingana na calculator ni dola 8000 ukiongeza na huo ushuru basi kuna kila sababu ya watu kutoshobokea huo mchongo.

Bongo Toyota itaendelea kutawala mpaka pale ccm itapotoka madarakani.
 
TRA ichukuliwe na DP World
 
Mshindani mwingine wa corolla ni nissan sunny gari moja nzuri sana sijui nissan wamefeli wapi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…