Hongera afande unastahili kupandishwa cheo

Hongera afande unastahili kupandishwa cheo

NostradamusEstrademe

JF-Expert Member
Joined
Jul 1, 2017
Posts
3,402
Reaction score
4,532
Iringa. Licha ya kutengenezwa baada ya kuharibika, Jeshi la Polisi, Kitengo cha Usalama Barabarani, Mkoani Iringa limezuia basi la Kimotco lililokuwa limebeba wanafunzi 62 na walimu saba wa Shule ya Msingi Camaldoli wilayani Mufindi lisiendelee na safari.

Jeshi hilo lilimelazimika kulizuia basi hilo baada ya kubaini halina mikanda ya abiria jambo ambalo ni hatari watoto.

Pia, basi hilo linadaiwa kuanza safari saa saba usiku kinyume cha sheria huku likiwa halijakaguliwa wala kupewa kibali cha kusafirisha wanafunzi.

Basi hilo limezuiwa wakati ikiwa zimepita siku chache baada ya wanafunzi 11 wanaosoma shule ya King David kupoteza maisha baada ya basi lao kutumbukia shimoni katika eneo la Mjimwema, Manispaa ya Mtwara Mikindani, Mkoani Mtwara.

Mkuu wa Kikosi cha Usalama, Barabarani Mkoani Iringa, Mosi Ndozero amesema ni kosa kisheria kwa basi lolote linalobeba wanafunzi kuanza safari usiku wa manane na bila kibali maalum cha kusafirisha abiria hao.

“Hii iwe ni onyo kwa mabasi mengine yote, ni marufuku kupakia wanafunzi bila kibali na kukaguliwa, lakini pia sheria hairuhusu safari za usiku.

“Basi hili nalichukulia hatua kali za kisheria ili iwe fundisho. Mmeondoka usiku wa manane vipi kama lingetokea lolote,” amesema.

Hata hivyo, baada ya basi hilo kutengenezwa kifaa kilichokuwa kimeharibika, ukaguzi wa polisi ulibaini halina mikanda kwa ajili ya abiria jambo lililomfanya Ndozero kuzuia lisiendelee na safari.

Mwalimu wa shule hiyo na mkuu wa msafara, Valence Ndembela walikiri walianza safari usiku wa manane kwa shinikizo la wenye gari.

Alisema awali, walikuwa wanawasiliana na wakala wa basi hilo, Agrey ambaye aliwahakikishia kuwa basi ni zima na limefanyiwa ukaguzi.

Kwa upande wake, wakala wa basi hilo, Agrey amesema japo wanafunzi hao walipakiwa kwenye mabasi mengine mawili, mkoani Dodoma watarejeshwa kwenye basi jingine la kampuni yao lililokaguliwa.
 
Sasa hapo anatakiwa apandishwe cheo kwa sababu gani! Si ametimiza tu wajibu wake!

Kwa hali hii basi madaktari wangepandishwa vyeo kila siku! Maana nao wanaokoa roho za mamilioni ya wagonjwa kule hospitalini!
 
Sasa hapo anatakiwa apandishwe cheo kwa sababu gani! Si ametimiza tu wajibu wake!

Kwa hali hii basi madaktari wangepandishwa vyeo kila siku! Maana nao wanaokoa roho za mamilioni ya wagonjwa kule hospitalini!
hayo ni mawazo yako mkuu lakini elewa angepewa kitu kidogo angeruhusu waendelee na safari count on me nimeandika hili bandiko mimi ni polisi wa usalama barabarani tunajua mambo yetu
 
mabasi kibao hayana mikanda, na yapo yanadunda tu.
walishindwaje kuzunguka nyuma ya basi wamalizane safari iendelee
 
Kama nakuona pale na tumbo lako lililovimbiwa rushwa.

Tokea barabarani mmeona mjifungulie uzi kupima maji?

IMG_20220729_082949_635.jpg


Hivi ajali gani zinasababishwa kutokuwepo na mikanda? Au ajali zipi zilizuiliwa na mikanda?

Nani asiyejua ajali nyingi zinasababishwa na ujinga, uchovu na usingizi ambamo humo hata nyie na wenzenu mnahusika mno?

Kwani mmewahi wapi kuyaangazia hayo kwa dhati?

Hata huyu mwenye hili basi si kuwa huenda alishindwa tu kuifika bei mliyompa.

Mnavyonuka rushwa ulikuwa muda sasa wa kuwabadili traffic wote kama vipi wawe FFU wajaribiwe wengine na wasiwe wanaachwa kudumu zaidi ya mwaka 1 hapo.

Ka rotation katika ngazi zote za traffic kangeweza kuwa na tija.
 
Back
Top Bottom