Hongera Benki ya CRDB

uncle

JF-Expert Member
Joined
Dec 10, 2007
Posts
325
Reaction score
184
Mojawapo ya taasisi nchini inayofanya vizuri kutokana na uongozi ni CRDB tokea ilipoanzishwa imekuwa na mafanikio makubwa na haswa kipindi ikiwa chini ya uongozi wa ndg kimei hadi Sasa ikiwa chini ya ndg Nsekeka.

Hii ni changamoto kwa taasisi nyingine katika sekta za kuhudumia wananchi ziige hii ya CRDB. Sina haja ya kutaja hizo taasisi wengi tunazijua na wenyewe wanajijua.

Hongera CRDB
 
CRDB ni benki ya hovyo na hivi ninavyoongea nimeagiza hisa zangu ziuzwe ,sitaki tena.Benki ambayo haiwezi kutoa taarifa sahihi kwa wateja wake hiyo ni benki gani? CRDB ukiomba mkopo kuupata ni kudra za mwenyezi mungu.Kuna upumbavu mwingi crdb na akaunti naenda kuifunga.
 
Chukueni tahadhari! Niliwahi kupewa card ya bank , gold card ! Kumbe mlemle ndani kuna mjuaji naye ana card nyingine ya namna hiyohiyo gold card!
Mlidokoa vya kutosha na mkome kunitumia emails zenu kuwa nirudi nimeshahama ninehama!
 
Kila Taasisi ina changamoto yake..
Japo Umeisifia kuijumla.. Ungesema wapi wanapo stahili kongole, ingependeza zaidi..
 
Hao wateja wenyewe siku hizi wanapukutika tu! Benki imejaa makato ya hovyo hovyo!! Habari ya mjini kwa sasa ni Equity Bank. Hakuna makato kwa mwezi! Na wanatoa mzigo mkubwa kuliko hao CRDB!
Nimekuelewa baba fulani wasalimi chako ni chako
 
Mtoa mada alikuwa kanywa copy ya k vant ndo moja yA madhara yake
 
UMEHAIDIWA SHS NGAPI?
 
Tatizo la CRDB ni 80% ya watumishi wake ni Nkya, Mushi, Mrosso, Tarimo, Kimaro, Urassa, Urio and the like.

Mojawapo ya legacy mbovu ya Kimei ndio hiyo, huwezi kuajiri 80% ya wafanyakazi kwa hoja za ukabila eti ni kabila lako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…