Hongera! Bodi ya mikopo HESLB ukizidisha malipo wanarudisha!

Hongera! Bodi ya mikopo HESLB ukizidisha malipo wanarudisha!

second9

JF-Expert Member
Joined
Jun 22, 2016
Posts
216
Reaction score
451
Wakuu,
Nimeona nitoe hii habari humu ili mtu asije kukata tamaa kwa maneno ya mtaani. Nilizidisha kama laki nne hivi kwenye kulipa deni la bodi ya mkopo. (HESLB)

Sasa ilipofika nataka kufatilia wanilipe kila niliyemwambia alisema niachane nao huwa hawalipi. Sasa siku moja nikaenda pale bodi nikajaza form za madai yangu. Baada ya miezi miwili jamaa wakatuma email nijaze upya taarifa kwenye mfumo wao mpya.... aaah hii nikaipuuza zaidi ya miezi 6 then siku nimefulia nikakumbuka nikajaza fomu online.

Huwezi amini kama baada ya miezi 4 au 5 nikashangaa muamala umesoma.

Hongera kwa bodi hii inaleta uaminifu ila tu muda wa malipo umekuwa mrefu sana wajitahidi kwenda speed ulimwengu wa technology huu.
 
Back
Top Bottom