Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 128,308
- 245,426
Hili jambo linapaswa kufanyiwa kazi na Viongozi wa Masumbwi Tanzania .
Zipo tuhuma kwamba mabondia wa Tanzania hawana uwezo , na huwa wanabebwa na waamuzi wa ndani kwa kuwapora ushindi mabondia wa kigeni , Hii ndio sababu kubwa ya mabondia hawa kutotaka kupigana Nje ya nchi , maana huko watachakazwa , maana Mwamuzi hatokuwa Mlundwa .
Ninao ushahidi wa bondia duni wa Tanzania Cosmas Cheka kupewa ushindi dhidi ya bondia mzuri kutoka Malawi katika pambano lililofanyika Morogoro , Cosnas Cheka alipigwa mwanzo mwisho lakini kwa Aibu ushindi akapewa yeye ! mambo kama haya nje ya nchi hayawezi kutokea , Hata pambano la Kwanza la Kidunda na Katompa , Ukweli ni kwamba Kidunda alipigwa ila Uzalendo ukatumia kumuokoa , nje ya nchi huwezi kufanya njama duni kama hiyo .
Mifano ya Matokeo ya kubebwa kwa mabondia wa Tanzania ni mingi na ya kutia aibu sana , hatuwezi yote kuiweka hapa
Nampongeza sana Mandonga kwa kupata ujasiri wa kupigana nje ya nchi na kushinda , hawa mabondia wa Kubebwa hawawezi kuthubutu .
Nakala : Chaurembo Palasa