Sungurampole
JF-Expert Member
- Nov 17, 2007
- 984
- 205
Katika mambo mazito mliyoyanadi katika ilani yenu ya uchaguzi mkuu wa 2010 ni elimu ya bure kuanzia chekechea hadi sekondari. Nasema hongera kwani licha ya kubezwa na sauti nzito za chama tawala ambao walitutaka tuamini kuwa haiwezekani serikali kutoa elimu bure kuanzia chekechea hadi sekondari, nyie mliendelea kusema ukweli kuwa inawezekana ili mradi tuwe na serikali makini. Nasema mmeonesha njia katika uongozi, kiongozi mzuri ni yule anayetoa hoja yenye manufaa kwa wale anaowaongoza na kuisimamia bila kutetereka hata kama mwanzo haitaungwa mkono.
Namkumbuka mwandishi mmoja, Robin Sharma - nguli wa mafunzo ya uongozi katika sura aliyoiita Leadership isnt a popularity contest alisema Being a leader isnt about being liked. Its about doing whats right
Inafurahisha kuona kuwa hoja yenu ya elimu ya bure hivi karibuni imepata washabiki wapya tena kutoka makada wa chama tawala. Lowasa, waziri Mkuu amekuwa wa kwanza kufunuliwa ukweli na usahihi wa hoja hii, naye kwa mujibu wa maelezo yake ya karibuni huko Babati ambako alisema anaamini kutoa elimu ya bure hadi sekondari inawezekana(Hongera kwa kuto kuwa mnafiki katika hili). What an about turn! Sitashangaa kama kufika 2015 watakuwa wamefunuliwa wengi zaidi na mengi zaidi kutoka ilani yenu ambayo mwanzo waliyabeza na kuyapiga vijembe. Ombi letu kwenu - endeleeni kuiboresha ilani yenu kuelekea 2015 sisi wananchi makini tunafuatilia kwa karibu mambo haya na kamwe hatutadanganyika na hadaa za wapinzani wenu. Ukifuatilia sarakasi za Tanesco kila kukicha utagundua kumbe hata bei ya umeme inaweza kushuka sana na kumpunguzia ukali wa maisha mtanzania wa hali ya chini ili mradi ufisadi ulioko uondolewe. Swali ni je, wenye hatamu wanaweza kuondoa ufisadi katika serikali na mashirika yake.
Natamani Nape na Kinana nao watokewe na muujiza uliompata EL ili wawaambie wananchi wa Kigoma (waliko sasa) kuwa nao wameuona mwezi na elimu ya bure hadi sekondari sio ndoto za CDM tena bali ukweli wa wote wasiopenda uongo- wasiogope kula matapishi kama hawana budi, hii haitakuwa mara ya kwanza, kwa sasa tumezoea na mifano iko mingi, leo wanabeza hoja na vijembe juu, kesho wanaiunga mkono asilimia mia (kama siyo wao vile)
CDM tupeni hoja na maeneo mengine, huenda mkawatia kiwewe wakatuboreshea maisha hata kabla ya 2015.