Hongera Chid Benz kwa ujio mpya zingatia haya ili usirudi ulipotoka, asante Diamond na AY

Leak

JF-Expert Member
Joined
Feb 22, 2012
Posts
52,916
Reaction score
43,505
Wasalaam wanajamvi.
Kati ya watu ambao hawakufiri kama msaanii Chid benz angeweza kurudi vyema kwenye ulingo wa muziki Mimi ni mmoja wapo maana nilihisi kama huyu mtu amesha changanyikiwa na amepoteza uwezo wa kufikiri au kukaa chini akatunga wimbo mzuri tena.

Pengine mwenendo wake na tabia zake zilimponza na sasa amejua pakurekebisha. Chid Benz ni kati ya wasanii waliopendwa na wengi na alipata mafanikio makubwa kupitia mziki wake na akabweteka na kujisahau!

Ujio wake mpya umenifurahisha sana na hakika tunaanza kumuona Chid Benz yule wa wimbo kama" Dares-salaam stand up" na nimefarijika sana kumsikia karudi rasmi na huyu ndio Chid benz ambaye tumekuwa tukimfahamu.

Wanajamvi hasa wale wapenzi wa burudani kama mmepata nafasi ya kuusikiliza wimbo wake unaoitwa "Mpaka kuchee" ambao amewashirikisha Diamond na Ay mtakubaliana nami kuwa huyu ndio Chid Benz mwenyewe maana mule ka rapu vyema naona sasa yuko serious!

Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni ...Diamond anajua kutumia nafasi anazopewa hasa kwenye kuimba, kwakweli kwenye wimbo huu kaimba vizuri sana na kautendea haki wimbo huu!Hata Ay mzee wa biashara ametenda haki nusu afunike.... kwakweli walijipanga big up sana kwa zawadi hii.

USHAURI KWA CHID BENZ

Kuna mambo ambayo amekuwa akifanya Chid benz na huwa kera wengi hasa sisi mashabiki wake mfano ...Kupigana hovyo,Kupiga hovyo,Matumizi ya madawa na bangi
hayo inabidi aachane nayo maana yanamchango mkubwa kuharibu muziki na kipaji chake.

Hawa alio imba nao ndio wanaweza kuwa muongozo wake hasa Ay anaweza akamsaidia sana kama akiamua kuwa sambamba nae.
Nivyema akaangalia aina ya marafiki ambao amekuwa nao siku zote ambao wamempelekea kuzama kwenye madawa inabidi awapunguze na afanye muziki sasa.

Namtakia kila la kheri kwenye safari alio ianza upya.

Karibuni wanajamvi.....
Mpaka kuchee-Chid Benz feat Diamond and Ay
 
Sijasikia huo wimbo ngoja nitafute
 

Anatafuta hela ya Sembe aendelee dozi


Sent from my iPad Air using JamiiForums
 
Watu hawataki amini kuwa watu wanabadilika, Chid kaona alipotea ndo maana amerudi
 
Haya banah! Ila muziki wa Bongo bado sana. Huyo diamond bado ana changamoto nyingi sana kwenye muziki, JK anamsaidia saidia na viji promo, anajifanya yuko ki mipango mipango, ngoja wakati wake ukifika tuone na yeye ata pambana vp na michosho ya muziki huu wa bongo. Hata AY mwenyewe hana lolote la maana, kuna kipindi alikuwa anaongea ongea ki mipango, kaamua kurudi shule. Muziki bado sana bongo hii, japo kuna viji hatua vina sogea sogea
 

Aiseeee
 
Wamsapoti wabeba sembe na watumiaji wenzake
 
Nyimbo ya kawaida sanaa..

Ya kawaida ila inaweza ikahit ukashangaa,kumbuka yumo Dangote umo...Dangote ana nguvu sana sasa hivi kiasi kwamba akisimama na wewe inaweza ikawa hamna hamna mara imo....Kerewa kerewa ya Shetta wakati inatoka niliona ya kawaida haitafika popote,ila hivi navyokwambia imeingia kwenye top ten ya radio tatu kubwa za Nigeria na amepata mkataba wa matangazo na dstv...shiit happens man!
 
OMG huyu Chidii???? Maskini kabaki kichwa tu..

Kabaki kichwa kwa kweli ila ukichokoza hapo hautaamini kama ni mteja jinsi watu walivyobalikiwa mkono wa ajabu,utaelewa kwa nini wanamuita chuma cha reli nondo.
 
Kabaki kichwa kwa kweli ila ukichokoza hapo hautaamini kama ni mteja jinsi watu walivyobalikiwa mkono wa ajabu,utaelewa kwa nini wanamuita chuma cha reli nondo.

Hahaha Matumbo bana najua ana nguvu ryt but mwili unapotea ameanza kuwa na Muonekano wa kiteja too bad.. Chidi anapendeza sana akiwa mnene
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…