Mwiba
JF-Expert Member
- Oct 23, 2007
- 7,607
- 1,750
Napenda kutoa hongera za dhati kwa Chama Cha CUF - Chama Cha Wananchi mimi ikiwa ni mmoja wapo wa hao wananchi ,kwa kufanya uchaguzi na kuumaliza kwa busara kabisa ,tunajua anaeshindwa haachi kulalamika hata Maximo nae hulalamikia wachezaji wake.
Napenda nichambue hoja za msingi za baadhi ya watu ambao wana msimamo tofauti na kwamba matokeo ya uchaguzi wa viongozi wa CUF hayaridhishi japo wanashindwa kuweka wazi ni wapi hayaridhishi.
Hoja ya kubadili viongozi:
Kila pahali panapotakiwa kuongozwa hua kuna utaratibu wa kuchagua viongozi na utaratibu wa cuf ni kama wote tulivyoona tangu mwanzo mpaka hapa tulipo,kama kulikua na haja ya kubadili uongozi ni kwa kura kupitia wajumbe sio vyenginevyo hivyo kama matokeo hayaridhishi ni hawa wachache hawakuridhika sio wananchi wote!
Hoja ya kutokua na imani:
Wengi kati ya wanaotoa maoni yao huja na hoja ya kutaka vijana waongoze, jamani hii dunia ya leo kama kila kitu twataka chende kwa mabavu ya vijana bila busara za wazee na hikima hatutafika pahali, hili lazima tulijue!!
kweli twahitaji nguvu mpya lakini mtumzima dawa na hawa ni wazoefu wa mikiki na dhoruba na mpaka sasa ni wachache wanaolalamika kuhusu ungozi wao mi nadhani tungewapa sapoti ya kweli ili tujivue katika janga tulonalo. viongozi wa juu wa CUF ni wenye uwezo mkubwa tu na wenye hamu ya kuleta maendeleo ya kweli katika nchi yetu na wanaokubalika kote Tanzania na kimataifa, ukiona jinsi wananchi wanavyo wapokea vizuri wanapokua katika ziara zao kote nchini ndio utaamini kweli wananchi wanaimani kubwa na hawa viongozi, tizama mikutano, sikiliza hutuba zao jinsi zinavyowagusa mojakwamoja wananchi halafu useme hawana imani nao si ukweli hata kidogo ni kutaka kupandikiza chuki na kukivuruga Chama halafu wakae pembeni wachekelee.
Hoja ya kutofika popote;
Kwa asietaka kuona haoni japo sote twatambua kama CUF ndio tegemeo la mabadiliko Zanzibar na Tanganyika kwa ujumla na ndio chama pekee kilichoweza kutoa upinzani wa kweli na hata kuifanya ccm iweze kubadili baadhi ya sera zeke na uonevu wa waziwazi unaoendelea, kwa miaka 16 CUF imepiga hatua kubwa na sasa MTanzania anaweza kutoa maoni na hata kuikosoa serekali kupitia chama!kuweza kua na wabunge na wawakilishi wanaotoa upinzani katika serekali zote mbili hii pia ni hatua na sasa tunaona baadhi ya mambo yanayoendelea ndani ya baraza la wawakilishi na Bunge ni juhudi za CUF kuitetea Zanzibar na Tanganyika mpaka kuwafanya wawakilishi na Wabunge wa CCM kujua kwamba hichi ni chetu na tukisemee hii pia ni hatua!
Hoja ya kupigiwa kura:
Hoja hii ni ya msingi sana kwani tangu mwaka 2000 CUF wamekua wakipata kura kutoka kwa wanachama wa vyama vyengine mpaka kutoka katika chama tawala! mimi kama mwananchi niliepiga kura 2000 na 2005 najua ya kwamba CUF inakubalika na wananchi walio wengi na wanapata kura hata kwa wana CCM tatizo ni jinsi ya kuzilinda!
Mimi napenda tujitahidi kuisapoti CUF kama chama Kikuu cha Upinzani na kilicho na hamu kubwa ya kubadili hali ya nchi yetu kiuchumi na kimaendeleo, nimuda wa kukaa pamoja kujadili nini cha kufanya kuisaidia CUF kushika uongozi nasio kukilalamikia kwa kurudisha viongozi wake katika kukiongoza chama.
Mapambano yanaendelea.

Last edited: