hongera Halmashauri ya Mpanda

ngoshwe

JF-Expert Member
Joined
Mar 31, 2009
Posts
4,131
Reaction score
937
Nimevutiwa na jinsi Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda ilivyojipanga kwa maonesho ya Nane nane hasa kwa kuwa na mfumo wenye kuwezesha mnyororo wa thamani (value chain) kwenye kilimo. Japo ipo mbali na mji mkuu wa nchi, Halmashauri hii iliyopo mkoa wa Katavi imeweza kuandaa vituo vya kuendeleza wakulima katika skimu ya kilimo ya Mwamapuli,kuna soko na kituo cha habari, trekta, miundo mbinu ya umwagiliaji, Saccos, kisima cha kuvunia maji nk. Pia wameweza kuandaa kitabu "kiongozi cha Mkulima" ambacho kinamsaidia mkulima badala ya kutegemea zaidi mtaalamu wa Ugani ambae kwa sasa ni vigumu kumfikia kila mkulima kwa wakati. Halmashauri zote nchini zingekuwa makini na kuiga yale yanayofanywa na wengine hakika kilimo kingeboreka kwa kuongeza tija, thamani na bei nzuri kwa maana ya kutekeleza Kilimo Kwanza.
 
Hongera sana, sasa tunataka kuona hayo kwenye maisaha ya kila siku ya mkulima...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…