Hongera HESLB kuongeza muda maombi ya mkopo, tatizo ni RITA kuchelewesha kutoa au kuthibitisha vyeti vya kuzaliwa au kifo

Hongera HESLB kuongeza muda maombi ya mkopo, tatizo ni RITA kuchelewesha kutoa au kuthibitisha vyeti vya kuzaliwa au kifo

TRAT

Member
Joined
Nov 29, 2022
Posts
73
Reaction score
160
Sitachoka kuwalalamikia RITA, unatuma cheti cha kuzaliwa walichotoa wenyewe, wanakaa nacho zaidi ya wiki 3, baadae wanakujibu picha ya kivuli haionekani vizuri.

Wanakwambia kitume upya. Ukishakituma baada ya siku kadhaa wanakujibu cheti walichotoa wenyewe eti hakiko kwenye orodha (hakijarekodiwa), omba upya.

Unaomba tena, siku kadhaa zinapita wanakujibu tayari kachukue cheti chako ofisi ya RITA wilaya.

Ukienda huko wanakuomba viambatanisho upya na risiti ulizolipia foleni kubwa kweli. Baadae wanakujibu bado hakipo kwenye orodha njoo siku nyingine, ukienda tena watakujibu bado, ukienda siku nyingine watakujibu leo siyo siku ya kuchukua vyeti.

Ukishakipata tena unaambiwa ingia kwenye mfumo tuna tena kivuli ili kiwe verified kwa kugongwa muhuri.

Hapo unaomba wasije kukwambia picha haionekani vizuri. Mambo ni hivyo hivyo hata kwa hati ya kifo.

Wiki 2 mlizoongeza bado zinaweza kwisha baadhi ya waombaji wasikamilishe.

Tatizo kubwa zaidi watendaji ofisi za wilaya wana uwezo mdogo wa kiutendaji.
 
Back
Top Bottom