Zanzibar 2020 Hongera Hussein Mwinyi kuutangazia Umma kuwa hutaki ushindi wa kura za wezi au wizi

Zanzibar 2020 Hongera Hussein Mwinyi kuutangazia Umma kuwa hutaki ushindi wa kura za wezi au wizi

Shocker

JF-Expert Member
Joined
Sep 15, 2012
Posts
1,958
Reaction score
3,890
Hongera sana kwa kuutangazia Umma wa Tanzania kuwa hutaki ushindi wa kura za wezi au wizi, ni sawa kwa kuanza kuwatahadharisha wanaopanga kukuharibia pepo yako, ama hapo umetoa kauli nzuri ambayo Inshaallah isiwe na shaka ndani yake.

Huku ni kujipambanua na mbinu zilizokuwa zinatumika kuwaweka viongozi madarakani na kama nilimsikia Magufuli akigusia haki itumike, katika kupata mshindi halali bila ya wizi.

Je, mnajua maana yake watu hawa kujitenga na kura za wezi? Kikinuka watakaobeba msalaba ni tume ya Uchaguzi na viongozi wa vikosi watakaokubali kuingizwa mjini na mitego ya CCM matumbo.
 
Hongera sana kwa kuutangazia umma wa Tanzania kuwa hutaki ushindi wa kura za wezi au wizi, ni sawa kwa kuanza kuwatahadharisha wanaopanga kukuharibia pepo yako, ama hapo umetoa kauli nzuri ambayo Inshaallah isiwe na shaka ndani yake.
Kumbe anajua kura za aina hiyo zipo na zimewahi kutumika. Vizuri. Lakini hayo ni maneno matamu kwani aliyeshika mpini si yeye ni JPM na watu wake.

Wengi tunasahau, Kikwete alisema CCM haitamfia mikononi mwake-akamkata Lowasa na kule Zenj wakamuibua Jecha. Mtihani mkuu wa JPM utakuwa Zanzibar.
 
Hongera sana kwa kuutangazia umma wa Tanzania kuwa hutaki ushindi wa kura za wezi au wizi, ni sawa kwa kuanza kuwatahadharisha wanaopanga kukuharibia pepo yako, ama hapo umetoa kauli nzuri ambayo Inshaallah isiwe na shaka ndani yake...
Kwa nyomi lile la Maalim. Nahapo ni Unguja makao ya CCM.

CCM haijawahi kushinda Maalim Seif.
 
Yeye anawekwa na CCM. Atake asitake kwa sababu yule ni MTU wa bara
Mtu wa bara hawezi kuwa Rais wa Zanzibar Mkuu ni katiba ya SMZ inasema hivo sio maneno yangu. Baba ake amekuwa Rais wa Zanzibar maana yake na yeye ni Mzanzibari.
 
kweli aisee..... Mwinyi na JPM ni dhahiri wanawaangushia jumba bovu Kaijage na mwenziwe wa Zanzibar pamoja na Sirro.
wakiingia kichwa kichwa na kuharibu halafu kupelekea intervention ya ICC, wataliwa hivyo vichwa mchana kweupe!!
 
CCM Zanzibar wameshashindwa,na mwaka huu watashindwa vibaya sana. Dr Hussein Mwinyi ni mtu mstaarabu amehamua kujitenga mapema na uhuni wowote ule Ila aende mbali zaidi wakimtangaza kwa mabavu akatae wampe hiyo nchi Jecha aiongoze.
 
Back
Top Bottom