Sawa, Bajeti ya tanzania inatokana na matumizi, elewa kwamba budget sio mauzo ya Taifa lakini kama tunapata share ktk miradi yetu bank zitatupa mtaji wa kuchimba dhahabu kwa kutumia credit ya hao Barrick. Ndivyo walivyofanya Botswana na nchi nyinginezo..Ebu jiulize inakuwaje Bank za dunia zinaweza kutupa mikopo na asilimia 45 au 30 ya bajeti yetu kwa matumizi ya ujenzi wa miundombinu kwa makubaliano ya kulipa interest bila ushuhuda wa fedha hizo kuzalishwa lakini Bank hizo hizo watunyime billioni 600 kwa biashara inayoonyesha faida. Mkuu ni bank hizo hizo zimeweza kuwapa barrick billioni 600 bila kuwa na dhahabu mkononi watashindwa vipi kutupa sisi wenye dhahabu tukishirikiana na Barrick!..Mkuu,
Unachokiomba na kukipendekeza naona kama ndoto vile kwanini. Mfano miradi ya uchimbaji dhahabu you need a huge capital let say around 600 Billion (assume). Bajeti ya Tanzania tu ni Trilioni 3 of which 30% of it comes from donors. Sasa nikuulize capital ya 600 Bilion utazitoa wapi? Tungelikuwa na maadili kusave serikalini tungeliweza kufanya unayoyapendekeza ila serikali za Tanzania matumizi kwenda mbele. Budget ya serikali inakuwa kila kukicha. Waarabu walikuwa wajanja walikuwa wanasave huku jamaa wanachukua mafuta kwa ubwete. Hadi walipohakikisha wameshakusanya mtaji wa kutosha wakaamua kuwa wanashare na wazungu (50-50 agreement). Sisi tunachokipata tunatumia hilo unaloliwakilisha halitawezekana labda serikali ya JK ikubali kufunga mkanda na wapinzani pia.
What next ?
Sema mfumo wenyewe ndio unatugandamiza sisi, mfumo ambao unatumika kwao wakitumia mashirika yao wanataka kuutumia kwetu ambao hatuna mashirika yale yale. Leo hii Barrick wakichimba dhahabu Canada kuna tofauti kubwa sana ya kimapato na mafao baina yetunna canada kwa sababu kila mauzo ya Barrick yanaingia ktk bank zao, mzunguko unakuwepo ndani na mikopo itatolewa kwa wafanyabiashara wengine, mishahara matumiz ya manunuzi na kadhalika lakini kwetu sisi Barrick wanakuja na kila kitu kutoka nje hadi accounts zao. Tunachofaidika sisi ni kiduchu kabisa labda hiyo mishahara na umeme maanake hata mafuta wanaleta yao nahayalipiwi kodi. karibu kila kitu wanachonunua Barrick hakina kodi sisi tunafaidika vipi na mauzoi ya Barrick kama sii hiyo ruzuku tu?