ACHENI JAKAYA KIKWETE AISHI KWENYE MABAWA YA MIDEGE ANGANI AKICHAGUA ILMRADI GHARAMA YA KODI ZETU KUIFADHILI MIRADI HIYO HAIZIDI ROBO YA TIJA TUNAYOVUNA KWENYE MAPENZI YAKE HAYO!!!
Hivi PakaJimmy, huenda huyu mwenye bandiko lake akawa ni Rweyemamu wa Ikulu kule Magogoni, Katibu Mwenezi na Propaganda CCM au ndio tuseme Zilipendwa Mzee Tyson Wassira Waziri wa Uhusiano leo hii kaamua kutoka Ki-Doti-Komu vile nini??
Tathmini ya huu Mradi wa ziara ya Mhe Kikwete Mi-Wizarani kamwe haitofanywa na akili za kilabuni hivi; tutakwenda mbele kidogo na kutaka ripoti iliyoandaliwa baada ya kutumia vigezo vya kisayansi (Project Monitoring and Evalution) ili kubaini kwamba tangu anapanga ziara hii.
Ni sharti JK atujibu kwa mtaji wa kodi zetu anazoendelea kutumia hivi sasa katika 'Kikwete Tembelea Wizara Project' (KTWP) na wal si kutupigia kelele za kishabiki hapa; huko kwenye siasa za kishabiki Vijana hatumo bali ni kwamba TIJA tu ndio tuwekewe mezani kweupe. Washiriki wa KTWP watujibu maswali kama vile Kikwete: (1) alikua na makusudio yepi, (2) kakuta hali halisi ikoje, (3) hali hiyo inajilinganisha vipi na kipinda cha mara ya mwisho mradi kama huo ulipotendeka, (4) Wa-Tanzania tumelazimika kuwekeza kiasi gani katika hiyo Month-Long Kikwete Project na iko wapi thamani ya kodi zetu mle????
Dr Bila ripoti tunaomba tangu ziara na familia yako mbugani na kote huko mikoani. Wapinzani na wabunge wote kwa ujumla nanyi tutawabana sana juu ya jinsi gani Viongozi Waandamizi wanavyotumia kodi zetu na TIJA za wazi zinazopatikana kwenye kile watendalo tukilinganisha na gharama iliotumika. Tukizingatia nidhamu kama hii tangu ikulu hadi nyumba kumi mitaani kwetu basi wananchi tutaona ACCOUNTABILITY wa hali ya juu!! Huko nyuma JK ameripotiwa kuwa na ziara nyingi sana na hata wakati mwingine kudaiwa kuwakera walipa kodi.
Kwangu mimi sitojali ziara zake ni nyingi kiasi gani ba ni thamani ya tija iliyopatikana ukilinganisha na gharama tulizowekeza mle. Tena mimi nitamuunga mkono sana JK akiweza basi kila siku awepo tu kwenye pipa angani kila kukicha ilmradi UNPOLITICISED WATCHDOG POLITICAL GROUPS AND PARLIAMENT wanaturidhisha katika hili bila swali kubaki kichwani mwetu.
Tunasupibi ripoti bungeni juu ya matumizi kwenye mradi huu na vile vile kwenye hotuba ya mwisho wa mwezi akajikite katika TIJA zenye kugusika na kuonekana tulizozivuna kwenye KTWP. Hatutaki blaa blaa na longo longo nyingi za mwaka wa 47 ambayo ndio haswa imetunashisha kama taifa kwenye huu umasikini gundi mabegani.
Mhe Kikwete kama CEO wa Tanzania kwa sasa, kama angelikua anaongoza kampuni ya kibiashara lazima angelazimika kuridhisha Wajumbe wa Bodi (Wahe Wabunge, nchi wahisani na Asasi za Kiraia husika) na haswa wamiliki wa kampuni (sisi wananchi) juu ya kila atendalo na faida ya kuonekana bila siasa, kwa nini ishindikane kwa ngazi ya taifa endapo kweli hatukusudii kuja kupata misaaada to Rwanda au hata Kenya kutupa LIFTI KWENYE NDEGE YAO toka kwenye hatari Libya????