Huu mto Ndumbwi ndio mto unaoingia Bahari ya Hindi Sambamba na nyumba ya marehemu Gertrude Lwakatare. Ukingoni mwa mto huu karibu na nyumba hiyo vilibuniwa viwanja na matapeli wa ardhi wilaya ya Kinondoni na Kuwauzia watu walioanza kujenga kinyume na sheria za nchi kuhusu Mazingira.
Kilio cha wanamazingira kuhusu uharibifu wa sehemu hiyo ambayo ni Mazaria ya Samaki kilisikika na NEMC na wahusika wengine wakachukua hatua na kuvunja uzio uliokuwa umejengwa sehemu ile. Kwa hatua hiyo hatuna budi kuwapa hongera!
Kwenye mto Ndumbwi huo huo kuna daraja lililojengwa kwa gharama nyingi na liko karibu na nyumba ya marehemu Apson aliyekuwa mkuu wa usalama wa Taifa na ndio maana daraja hilo hujulikana kwa jina lake. Daraja hili muhimu liko hatarini kubomoka iwapo hatua za haraka hazitachukuliwa kuwasimamisha watu wanaolima mahindi na mazao mengine pembeni mwa mto nyuma ya bakery.
Kilimo sehemu hiyo kina fanya mto ukijaa kufurika mpaka kwenye barabara hivyo kuhatarisha uimara wa daraja.
Kuwasimamisha wanaolima kando ya mto na kuchimba mchanga kutapunguza gharama za hilo daraja hapo baadae.
Wahusika hawana budi kulishuhulikia suala hili kwa umuhimu unapata hilo na kwa haraka iwezekanavyo.