Hongera kwa wana Serengeti na wana Mara kwa ujumla kwa kitoweo hiki!!

Manstone

JF-Expert Member
Joined
May 12, 2013
Posts
516
Reaction score
315
Habari wana Jf!
Shukrani Ziwafikiwe Wana Mara Wote Hasa Kwa Ndugu Zetu Wanaserengeti Kwa Kutupokea Vizuri,
Tuliandaliwa Chakula " UGALI" wa mtama uliochanganywa na unga wa mihogo na kitowewo aina wanayoiita " KIMORO".
Kitowewo hiki kilikua kitamu sana japo kilikuwa na harufu kali, ambayo haiwezi kusababisha uiache kuitumia kulingana na utamu wake.
Niliwauliza wenyeji hii nyama ni ya nini? na kutujibu ni nyama ya pori ambayo huanikwa juani katka vipande vya saizi tu na kukaushwa kwa jua pamoja na chumvi huko huko porin na kuleta vipande vilivyokaushwa.
Niipenda sana kitowewo hiki, na kufungashiwa vipande viwili vya nyama hizi kiukweli zilkua zikionekana kama ngozi.
Baada ya kuondoka nikajiuliza, je huko porini wakiua simba au fisi wakiikausha utaijuaje?
 
wapenda kula kula kama wew hata mkilishwa simba sio mbaya
 
Ukishikwa nacho! Miaka 30 lupango. Nyara za serekali.
 
Hiyo kitu ni illegal na hapa unawachongea wenyeji wako wa Serengeti ni vema ungekaa kimya hata hii mada ungeifuta.

Nyama pori ni nyara ya serikali, kuitumia inatakiwa uwe na kibali.
 
Hiyo kitu ni illegal na hapa unawachongea wenyeji wako wa Serengeti ni vema ungekaa kimya hata hii mada ungeifuta.

Nyama pori ni nyara ya serikali, kuitumia inatakiwa uwe na kibali.

mkuu hujui kuwa watu wana vibari kabisa vya kuwinda na wanafanya kazi hi kihalali.
 
mkuu hujui kuwa watu wana vibari kabisa vya kuwinda na wanafanya kazi hi kihalali.
Huko Serengeti watu wangapi wana vibali vya kuwinda?
Huko ni kwetu huwezi kunidanganya kwa lolote.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…