Hongera Mahakama kutengeneza Historia.

Ukitaka kujua uchafu wa wacongo wapangishie nyumba yako,utaona vituko vya kila aina, ndiyo hata wamemuharibu Kapuya hao wale wa bendi yake AKUDO

Na uchafu wa tz???????? kuua albino,, baba/mama kutembea na mtoto wake, mauaji ya kila siku,, ushirikina kukamatwa na viungo vya binadamu???? hao ni wacongo?????? next time usiongee usichokijua!!!!!!!!!!
 
Bado hainiingii akilin hii hukumu haiwezekan tena narudia haiwezekan baba na mwana kubaka toa papii na nguza peleka huyo kapuya
 
Mungu Wangu!!! ni kauli zinawatoka wanadamu? kufungwa wameshafungwa bado tunapigilia misumari jamani! ingekuwa ni baba yako amefanya kitendo hicho ungejiangaliaje kwenye jamii..? tusihukumu kiasi kama umefanyiwa wewe kitendo kile. kama ni kuwaombea waozee jela wameshinda basi jamni mengine aachiwe maulana.
 

na wewe tupe ushahidi kama walibaka kweli!,je uliwaona?,vinginevyo usihukumu!
 
watanzania wengi huwa ni wavivu wa kusoma ukifatilia hawa wote wanaoshabikia babu seya hawakufatilia mwenendo wa kesi toka iko kisutu ila wanachojua ni kusema kuwa babu seya hakubaka mlikuwa naye? au mlikua mnaishi wote?
 
Mahakama ya Rufaa nchini Tanzania imetupilia mbali ombi la warufani wawili Nguza Viking na mwanaye, ambao waliomba mahakama hiyo kufanya marejeo ya uamuzi wake wa awali wa kuwapata na hatia kama ambavyo hukumu dhidi yao ilivyotolewa na mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mwaka 2004.

Nguza Viking, maarufu kama Babu Seya na watoto wake watatu walihukumiwa kifungo cha maisha jela kwa makosa ya kubaka na kulawiti watoto.

Mwaka 2010, rufaa yao ilisikilizwa katika Mahakama ya Rufaa, na kuwaachia huru Nguza Mashine na Francis Nguza baada ya kuwaona hawana hatia katika makosa yote waliyoshitakiwa.

Baada ya rufaa hiyo, Babu Seya na mwanaye Papii Kocha walipatikana na hatia na hivyo kuendelea kutumikia adhabu ya kifungo cha maisha jela.

Tarehe 30 Oktoba mwaka huu, Mahakama ya Rufaa iliyoketi chini ya jopo la majaji watu, likiongozwa na Nathalia Kimaro, akisaidiana na Mbarouk Mbarouk na Salum Masati walisikiliza hoja za pande zote kuhusu ombi la kufanyika mapitio ya uamuzi wa awali wa mahakama hiyo.

Alhamisi, Mahakama ya Rufaa baada ya kufanya mapitio ikiwa imeketi chini ya majaji watatu, imeendelea kuwaona warufani hao wawili kuwa na hatia na hivyo kuendelea kutumikia adhabu yao.

Upande wa utetezi ukiongozwa na wakili wao Mabere Marando uliomba kupitiwa upya kwa uamuzi huo, ukidai kuwepo kasoro katika ushahidi uliowatia hatiani, ikiwemo kukosekana kwa mashahidi muhimu katika kesi hiyo.

Majaji walisema kuwa kuna uthibitisho kuwa warufani hao wawili waliwabaka watoto wa shule ya msingi mwaka 2003.

Kesi hiyo imewashtua mashabiki wa mwanamuziki Viking nchini Tanzania na kanda nzima ya Afrika Mashariki.

Mwanamuziki huyo mwenye kuimba nyimbo za Rhumba, ambaye ni mzaliwa wa DRC, ameishi Tanzania kwa miaka mingi na kuwa na mashabiki wengi.

Mwandishi wa BBC Ben Mwang'onda mjini Dar es Salaam anasema kuwa Nguza Viking na mtoto wake Johnson Nguza maarufu kama Papii Kocha ambaye pia ni mwanamuziki, walifika mahakamani hapo kusikiliza hatma yao.

Walionekana kuwa watulivu wakati majaji walipotupilia mbali ombi lao kutaka hukumu yao kubatilishwa.

Walihukumiwa kwa kuwabaka wasichana 10 wa shule ya msingi waliokuwa kati ya umri wa miaka sita na nane wote waliokuwa katika shule ya msingi ya Mashujaa wilayani Kinondoni mjini Dar es Salaam.

Wakili wa muimbaji huyo alisema kuwa mwanamuziki huyo hana matumaini tena ya kupewa rufaa kwani hili ndilo ombi lake la mwisho.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…