Kamgomoli
JF-Expert Member
- May 3, 2018
- 1,896
- 4,058
Kwenye mechi ya jana (Yanga VS TP Mazembe), Mwamnyeto alikuwa na kiwango bora sana. Hofu yangu ni je ubora huu aliouonyesha utaendelea? Maana pale Yanga kuna wachezaji wengi ambao ni maji kupwa maji kujaa, yaani hawana mwendelezo.
Leo anakiwasha kweli kweli, kesho madudu matupu! Mfano Tuisila, Moloko Faridi na Ambundo. Mwamnyeto anawajibu wa kupambana ili kuwa na mwendelezo wa kudumu.
Pili, Mwamnyeto anakaba kwa kuvamia kitu ambacho ni hatari kama anakutana na washambuliaji wenye akili na wajanja wajanja ambao wanaweza kumtaftia penalti au kadi nyekundi.
Tatu, Mwamnyeto anapenda kukokota mpira kupanda mbele halafu anabutua pasi mkaa au kunyang'anywa mpira kirahisi. Hii ni hatari km timu pinzani ina wachezaji wenye speed anaweza kuchomesha kirahisi sana.
Alichokifanya jana Mwamnyeto ndicho Wanayanga wanataka afanye mechi baada ya mechi km ilivyo kwa Dickson Job.
Nawasilisha.