Hongera Mwamnyeto lakini bado una machache ya kurekebisha

Kamgomoli

JF-Expert Member
Joined
May 3, 2018
Posts
1,896
Reaction score
4,058
Kwenye mechi ya jana (Yanga VS TP Mazembe), Mwamnyeto alikuwa na kiwango bora sana. Hofu yangu ni je ubora huu aliouonyesha utaendelea? Maana pale Yanga kuna wachezaji wengi ambao ni maji kupwa maji kujaa, yaani hawana mwendelezo.

Leo anakiwasha kweli kweli, kesho madudu matupu! Mfano Tuisila, Moloko Faridi na Ambundo. Mwamnyeto anawajibu wa kupambana ili kuwa na mwendelezo wa kudumu.

Pili, Mwamnyeto anakaba kwa kuvamia kitu ambacho ni hatari kama anakutana na washambuliaji wenye akili na wajanja wajanja ambao wanaweza kumtaftia penalti au kadi nyekundi.

Tatu, Mwamnyeto anapenda kukokota mpira kupanda mbele halafu anabutua pasi mkaa au kunyang'anywa mpira kirahisi. Hii ni hatari km timu pinzani ina wachezaji wenye speed anaweza kuchomesha kirahisi sana.
Alichokifanya jana Mwamnyeto ndicho Wanayanga wanataka afanye mechi baada ya mechi km ilivyo kwa Dickson Job.

Nawasilisha.
 
Hiyo point ya tatu hata mimi nimeiona amepoteza mipira mingi sana kwa kubutua mbele sehemu ambazo alitakiwa kutoa pasi clear kabisa
 
Muhimu tumewafunga mdomo makolo hayo mengine ni ya kocha na wachezaji wake.
Malengo ni kuwafunga midomo makolo au ushindi katika kundi lenu ?

Hivi timu ya Daraja la Kwanza inashindanaje na timu ya Ligi Kuu ?
 
Amekusoma kocha
 
Sio Mwamnyeto tu hata Djuma nao karudi kwenye ubora wake.
 
Mwamnyeto ni mzuri anapocheza nyuma ya kiungo mkabaji aina ya Bangala. Na hilo la kupanda mbele na kubutua, kuvamia wapinzani wake, nk. Uko sahihi kabisa.

Hata ile faulo iliyozaa goli, ilisababishwa na yeye mwenyewe baada ya kumvamia yule mshambuliaji wa Tp Mazembe.
 
Ila kabla ya mechi wewe ulikuwa mchambuzi uchwara ukiipondea yanga.
Ushindi wa jana haimaanishi mapungufu ya kina Tuisila na Maloko yameisha. Inawekana TP hawakuisoma vzr Yanga.
 
Sahihi.. Anacheza kwa presha sana.
 
Sahihi.. Anacheza kwa presha sana.
Jana ameisaidia sana timu yake kwenye mipira ya juu. Natamani kumuona akiendelea kucheza nyuma ya Yannick Bangala, kama walivyocheza jana.

Hakika utulivu ulionekana kule nyuma.
 
Pili, Mwamnyeto anakaba kwa kuvamia kitu ambacho ni hatari kama anakutana na washambuliaji wenye akili na wajanja wajanja ambao wanaweza kumtaftia penalti au kadi nyekundi

Kipindi nacheza mpira nilikuaga nawadhalilisha sana mabeki wa aina hiyo....

KUNA SIKU MA BEKI WAWILI WALIFANYA AMBUSH KWENYE MPIRA WA JUU NIKIWA KATIKATI YAO.. NILIWACHOMOKA HAWAKUAMINI WAKAGONGANA VICHWA NA WAKAUMIA VIBAYA SANA KIASI CHA KUSHINDWA KUENDELEA NA MECHI....
 
Vise versa is totally true, ulikutana na mbwenyenye si Mabeki visiki wenye uzoefu wa kazi na kujua akili yako inachowaza ni kipi kabla ya kuwatoka.

Messi alirusha masumbwi (ngumi) kule La Liga alipobanwa na kushindwa kufurukuta kabisa, sembuse wewe [emoji848][emoji38]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…