Siyo Hussein Nyika bali ni Hussein Mnyika. Ni jambo baya sana Mwana Yanga kutojua hata tu majina halisi ya Viongozi wako na hii inaonyesha dhahiri kuwa hata jana mlistahili ' Kufungwa ' kwani mna matatizo mengi ya yanoanzia Vichwani hadi Miguuni mwenu.
Kurudi katika aina ya Uchezaji wa Mchezaji wenu Papy Kabamba Tshishimbi nitamuelezea kwa namna mbili hasa za Kimchezo. Nikiri tu kwamba Tshishimbi ni Mchezaji mzuri na jana ameonyesha kuwa anaweza akaja kuwa Mchezaji mzuri. Ana karibia 85% ya Sifa zote anazotakiwa kuwa nazo Defensive Midfielder.
Tatizo lake.
Tshishimbi si mchezaji wa 90 minutes kwani ' Kiutaalam ' tu jana aliweza kuwa juu kwa dakika kadhaa lakini mara nyingi tenki lake la mafuta ( Pumzi ) ilikuwa inakata sana hali ambayo Kipindi cha pili alikuwa anapoteza mno mipira kwa kupiga pasi mfu au pasi ' msakizio ' hali ambayo ilimuharibia kidogo.
Changamoto Kwake.
Sawa tunamsifu kuwa Tshishimbi ni bonge la ' Mido ' ila tujiulize swali moja tu kwamba ile jana alicheza na aina gani ya Wachezaji? Nina uhakika tena wa 100% kwamba kama ile jana Simba ingewachezesha katika ' midfield ' akina Jonas Gerald Mkude na Said Khamis Ndemla huyu Tshishimbi asingeweza kuyafanya yale aliyoyafanya jana. Mkude na Ndemla ni wazuri sana katika ' Kukichafua ' katika ' Kiungo ' na kwa aina ya uchezaji wa Tshishimbi wangemsumbua na kumtesa mno.
Mwisho
Ili kuweza kusema kwamba Tshishimbi ni bonge la ' Mido ' hebu tusubiri angalau mechi kama tatu au tano za ' Ligi ' ya VPL ili tuone kama ataendelea hivi hivi au mambo yatabadilika. Na yawezekana pia jana Tshishimbi alionekana ' Kutakata ' pengine kutokana na ' mfumo ' mzima wa uchezaji ( namaanisha game approach ) ya ' derby ' ya jana ambao anaweza pia asiupate katika mechi zingine ambazo Yanga itakuwa inacheza. Kwa mfano mtake msitake kwa aina ya uchezaji wake siku ambayo Yanga itacheza na Azam huyu Tshishimbi atapotea mno kwakuwa Azam wana aina ya Viungo ambao ni very ' combative ' akina Himid Mao Mkami na mwenzake Salum Abukary ambao hawatakuwa wanacheza nae kama ambavyo jana James Kotei na Muzamiru Yasini walikuwa wakicheza nae.
Kuna Gazeti moja la Leo nimeona ' Mhariri ' kaandika kuwa Tshishimbi kampoteza Niyonzima kitu ambacho kilinishangaza mno na kuhisi kuwa huenda huyu Mhariri ameanza kufuatilia mipira siku za karibuni. Hawa Wachezaji wawili wote jana walikuwa na ' roles ' tofauti na ndiyo maana muda mwingi walikuwa hawakutani sasa kuwashindanisha ni jambo la ' Kipopoma / Kipumbavu ' kabisa.
Jana Niyonzima alipewa ' Jukumu ' la kuwa ' Play maker ' wa Timu ambapo alikuwa akionekana kila eneo la mpira huku Tshishimbi akipewa ' Jukumu ' kubwa la kuweza kusaidia hasa sehemu ya defensive ya Yanga na kuweza kumuanzishia mipira Thabani Skara Kamusoko na Timu iende. Kidogo huyo Mhariri angesema kwamba Kamusoko ' kamfunika ' Niyonzima ningemwelewa kwani ni ukweli usiopingika kuwa Kamusoko jana ' aliupiga ' mwingi mno na alionyesha kweli Yeye ni ' Injini ' Kuu ya Yanga.
Yangu ni hayo tu na kila la kheri ila nisiwe mnafiki au mchoyo wa kutoa sifa na nasema tena kuwa Yanga wa Mchezaji Papy Kabamba Tshishimbi hakika wamelamba ' dume ' na atawasaidia sana kumsahau haraka / mapema Haruna Fadhili Hakizimana Niyonzima.