Hongera precission air kwa kuanza kujitegemea(handling)

Hongera precission air kwa kuanza kujitegemea(handling)

Pdidy

JF-Expert Member
Joined
Nov 22, 2007
Posts
57,951
Reaction score
32,619
Ndugu zanguni si haba kuwapa hawa ndugu zetu wanaojaribu kujitoa katika soko la urtumwa la swissport;leo hii swissport wameanza rasmi kujitegemea kwenye handling ...kazi ambayo imekuwa ikifanywa kwa pesa nyingi zisizo na aibu na swissport...leo hii wamefungua milango kuonyesha jamii kwamba ule ukiritimba wa swissport kuwa kampuni pekee ya handling airport imekwisha...Hongereni sana sana na sana
WAZO

Katika biashara kuna mambo mengi ya ushinddani...na pia kuna upumbavu mwingi unafanyw na wachache nakuonekana kampuni nzima...labda cha kuwasaida kama mmeamua kuwaserious jitahidini kuwa makini katika mambo yafuatayo

1) EXCESS

Tayari kuna kampuni nyingi sana......,zimekuwa zikikosa mapato kutokana na excess baggage kuchukuliwa na watu badala ya kuingizwa moja kwa moja kwenye kampuni...hili ni kuwahimiza abiria wasikubali kutoa hongo kila walipapo hela za mizigo ya ziada.....lingine
 
Napinga airline kuwa na "handling services yake yenyewe" ila nakubali swissport kupata mshindani.
 
Kwa kweli ningefurahi kama Air Tanzania wangepata nafasi hiyo kwani kuwakaribisha Precisionair ni kuwakaribisha Wakenya - kwa namna yao Kenya airways imepewa nafasi ya kujipenyeza ndani ya nchi yetu kwenye viwanja vyetu jikoni kwetu - Je inawezekana kwa kampuni ya kitanzania kufanya hivyo Nairobi airport? Hivi hao wanaotoa vibali hawana macho ni vipofu??????????
 
Precisionair ni Kenya Airways sasa Serikali lazima iwe macho ingawa maji yakimwagika hayazoleki lakini kibali kikitolewa kinaweza kubatilishwa jamani tuwe na uchungu na nchi yetu watoto wetu watakuja kutulaumu........Serikalini mpo wapi? Nani anayetoa vibali?
 
Hili linaweza likawa wazo baya kibiashara kwani itaongeza gharama za uendeshaji kwa kuajiri watu wao wenyewe kufanya handling, vifaa vyao wenyewe, ofisi, maghala n.k., wakati ndege na mizigo yao ni michache.

Kama wanaanzisha kampuni ambayo itahudumia pia makampuni mengine ya ndege, hapo ndio inaweza kuwa biashara nzuri othewise wamekosea.

Mashirika mengi makubwa ya ndege duniani, kama American Airways, Delta Airways, South African Airways, Ethiopian, n.k., yanatumia makampuni binafsi ikiwamo Swissport kuwafanyia handling.

Kujitegemea sio lazima iwe ni uamuzi bora kibiashara, inabidi wawe waangalifu.
 
Kwa kweli ningefurahi kama Air Tanzania wangepata nafasi hiyo kwani kuwakaribisha Precisionair ni kuwakaribisha Wakenya - kwa namna yao Kenya airways imepewa nafasi ya kujipenyeza ndani ya nchi yetu kwenye viwanja vyetu jikoni kwetu - Je inawezekana kwa kampuni ya kitanzania kufanya hivyo Nairobi airport? Hivi hao wanaotoa vibali hawana macho ni vipofu??????????

Inaelekea wengi wetu hatujui maana ya Kuwa na common market ya jumuiya ya Afrika Mashariki; mara wakubwa watakapotia saini mkataba wa kuwa na soko la pamoja maana yake wanannchi wa nchi husika watakuwa huru kuishi, kuajiriwa na pia kuwekeza popote katika Jumuiya!! Sasa hao wakenya mnaowaogopa ndio wataingia kwa mlango wa mbele!!
 
Sawa Bulesi na siasa zako za common market lakini unawajua wakenya? Mwaka 1977 walitufanya nini? Historia hujirudia - mali zote za EAC zilibaki Kenya hawa ni marafiki wakati una shida tu wakimaliza wanachotaka toka kwako hawakujui!!!!! Hii ndio maana watanzania wengi hatupendi kile mawaziri wanakifanya lakini hatuna uwezo wa kupinga na ndio labda jukwaa kama hili tutasema wasipotusikia lakini tumesema.

Watanzania waliopata kuishi Kenya wanajua uchungu wa kukaa na kufanya kazi Kenya utake usitake Bulesi hatuwataki Wakenya tulazimisheni tu na mfanye mpendavyo nyie wenye nguvu tutabaki na unyonge wetu!!!!
 
Ndugu zanguni si haba kuwapa hawa ndugu zetu wanaojaribu kujitoa katika soko la urtumwa la swissport;leo hii swissport wameanza rasmi kujitegemea kwenye handling ...kazi ambayo imekuwa ikifanywa kwa pesa nyingi zisizo na aibu na swissport...leo hii wamefungua milango kuonyesha jamii kwamba ule ukiritimba wa swissport kuwa kampuni pekee ya handling airport imekwisha...Hongereni sana sana na sana
WAZO

Katika biashara kuna mambo mengi ya ushinddani...na pia kuna upumbavu mwingi unafanyw na wachache nakuonekana kampuni nzima...labda cha kuwasaida kama mmeamua kuwaserious jitahidini kuwa makini katika mambo yafuatayo

1) EXCESS

Tayari kuna kampuni nyingi sana......,zimekuwa zikikosa mapato kutokana na excess baggage kuchukuliwa na watu badala ya kuingizwa moja kwa moja kwenye kampuni...hili ni kuwahimiza abiria wasikubali kutoa hongo kila walipapo hela za mizigo ya ziada.....lingine

Swissport kwa ukarimu wao wameaazima vigi vya kuvutia matela ya masanduku! Ila vitoroli vyao vinaonekana vimetumika sana! sijui walivichukua hapo kenya
 
hapa maanake unamkaribisha mgeni akufagilie nyumba yako, akudekie na akutandikie kitanda.........SIKU MOJA ATAKUWEKEA BOMU KITANDANI.....!
 
hapa maanake unamkaribisha mgeni akufagilie nyumba yako, akudekie na akutandikie kitanda.........SIKU MOJA ATAKUWEKEA BOMU KITANDANI.....!

Kwangu ni uwekezaji mzuri. At least wataajiri watu wetu, kulipa kodi na charges zingine.

Tuna ubavu wa kufanya lolote - au ni maneno ya kizalendo tu? Hiyo ATC yenyewe - ndege ya mwisho alinunua Nyerere zaidi ya miaka 30 iliyopita na pia tangu Nyerere alipojenga terminal 2 DIA na KIA hakuna zaidi - utafikiri dunia imeacha kuzunguka
 
Kwa kweli ningefurahi kama Air Tanzania wangepata nafasi hiyo kwani kuwakaribisha Precisionair ni kuwakaribisha Wakenya - kwa namna yao Kenya airways imepewa nafasi ya kujipenyeza ndani ya nchi yetu kwenye viwanja vyetu jikoni kwetu - Je inawezekana kwa kampuni ya kitanzania kufanya hivyo Nairobi airport? Hivi hao wanaotoa vibali hawana macho ni vipofu??????????
hivi wewe huoni hayo madudu yanayofanyika air TZ, kweli kipofu....

kwani kenya air ways si ina miliki 49% tu, hamna ubaya wowote
 
Nakataa suala la kila kitu nchini kwetu tugawane na wageni, sielewi hii concept ya uwekezaji inachukuliwaje vichwani mwa viongozi wetu ..yaani inatia kichefuchefu!

Mi nilidhani uwekezaji ni kwa ajili ya vitu ambavyo sisi wazawa tumeshindwa kuvifanya aidha kwa sababu ya ukosefu wa mtaji na/au wataalamu na/au vifaa, lakini naona uwekezaji wanaoujua wao ni tofauti, na kwa hali hii tusitegemee kujikwamua kiuchumi maana hata vile vidogo ambavyo vingeleta ajira na kipato japo kidogo kwa watu wetu tunagawana na wageni au wazabuni!
 
tuwe wakweli kenya airways wako mbali sana kutoka tunapoongelea, wana daily flight from london Heathrew to nrb na haina ubabaishaji wowote kwa nini tusijifunze toka kwao badala ya kuwapinga wakati hatuna uwezo. Au lazima tujifunze toka kwa wazungu? Im afraid hata JF ikipewa tenda ya kuendesha ATCL pamoja na madongo yetu yote hatuwezi kufanya maajabu Unless we swallow the Truth (mother fucken) we can't unless we learn from elsewhere,..no matter where!!!!!!!!
 
Kwangu ni uwekezaji mzuri. At least wataajiri watu wetu, kulipa kodi na charges zingine.

Uwekezaji mzuri wakuleta vitela bomu vilivyotumika Kenya na kupakwa rangi ya kijani? Tanzania ni jalala la scraper?
 
hivi wewe huoni hayo madudu yanayofanyika air TZ, kweli kipofu....

Hapa ni suala la maamuzi ya nani awe nani na wapi salaam hizi zipelekwe kwa wale wanaoamua nani awe nani na akae wapi!

Tanzania bila wakenya inawezekana! hatudanganyiki!

YES WE CAN
 
Uwekezaji mzuri wakuleta vitela bomu vilivyotumika Kenya na kupakwa rangi ya kijani? Tanzania ni jalala la scraper?

Lini tulinunua kipya (ukiacha miaka ya Nyerere)? IPTL? Dowans? Mabehewa ya treni? Ndege za kukodi ya ATC? boti/meli vivuko gani vimenunuliwa vipya? Barabarani/bandarini kumejaa nini kama siyo magari & mitambo yaliyotumika!

Tanzania bila wakenya inawezekana! hatudanganyiki! YES WE CAN

Nasema Yes we can't. Mfano mdogo tu - bidhaa kama Tanzanite na sangara bila Kenya zisingepata soko ulaya.
 
Back
Top Bottom