Hongera Prof. Kabudi kwa umahiri wa kusoma kwa kufuata vituo kwa usahihi

Hongera Prof. Kabudi kwa umahiri wa kusoma kwa kufuata vituo kwa usahihi

lulu za uru

JF-Expert Member
Joined
Aug 7, 2015
Posts
2,557
Reaction score
3,221
Jamani hakuna aliyekamilika ila sifa ya MTU apewe akiwa hai aisikie. Profesa Palamagamba Aidani Kabudi anajua kutamka matamshi ya lugha sana, kusoma kwa kufuata vituo zile nukta, mkato, koma, funga na fungu semi na alama nyingine akipewa paragraph akusomee sio siri utafurahia sana aina ya usomaji wake. Ana sauti ya kimamlaka sana.

Hongera hapa lazima watakumbushia ile ya kutolewa jalalani ila tukumbuke. Hakuna mkamilifu chini ya jua.....
 
Weka na video basi! Au unadhani watanzania wote tunafuatilia hilo tukio live?
 
kawataja wenye vyeti feki wazee wa unanijua mi nani?
 
Mbona mnapenda sana kujikomba komba?hicho unachokisifia hapa anakifanya mwanangu wa darasa la tatu wewe unakuja kumsifia mzee mwenye mvi kichwani?

Upo sawasawa kichwani kweli wewe?Lete hapa ni jambo gani alilowahi kusimamia na uprofesa wake likaleta impact kwa taifa siyo hizi sifa za kitoto unazomwaga.
 
Kwa hiyo professor anapimwa kwa kufuata vituo?
 
Ni kweli ana sauti ya ki-mamlaka.Uwezo wake wa kuongea ni wa juu sana.ndiyo maana marehemu alipa hiyo wizara.

Ila sina uhakika na utandaji wake wa kazi.sababu kusemasema ni kitu kimoja na utendaji kazi wenye matokeo ni kitu kingine.Nimejifunza kwa Husein Mwinyi wa Zenji.sauti yake ni ya chini sana ila matokeo yake ni makubwa sana.
 
Hadi profesa anasifiwa kwa kusoma taarifa ya kiswahili hii aibu ya mwaka kabisa, hii nchi inashida gani hasa, mtu mzima kabisa na akili utamsifia profesa kwa kusoma taarifa ya kiswahili
 
Back
Top Bottom