Hongera Rais kwa kupata nafasi ya kuonesha ushujaa wako

Hongera Rais kwa kupata nafasi ya kuonesha ushujaa wako

Mc PIPI

JF-Expert Member
Joined
Feb 25, 2020
Posts
325
Reaction score
442
Napenda kutanguliza salamu zangu kwenu.

Niwakumbushe tu fasili ya neno shujaa ni kuwa ni mtu anayefanya mambo makubwa mazuri yasiyotegemewa katika kipindi au sehemu ngumu.

Ni hivi Sasa tangu uanze mchakato wa kura za maoni kila kuchapo Kuna malalamiko mbalimbali kutoka maeneo mbalimbali tena mengine yana ushahidi kabisa.Malalamiko hayo ni kuhusu michakato hiyo kugubikwa na vitendo viovu vya RUSHWA. Naweza thubutu kusema 98% Kama si 100% kila Jimbo vimeshuhudiwa vitendo hivi vya rushwa na hivyo matokeo yote kutokuwa halali.

Kwakuwa Nina imani mno na dhamira ya dhati ya Rais juu ya kumfanya TANZANIA isiyokuwa na RUSHWA,na ndiyo maana unajaribu kuhangaika hapa na pale hata kuamua kuja na kanuni za uchaguzi ndani ya chama ambazo zilikemea mno vitendo hivyo,lakini watu hawakutoa ikawa hata kidogo na hizo kanuni.

Sasa,una nafasi ya kuwashangaza watu kuwa ukisema kweli umemaanisha,kazi ni rahisi tu,ni mwendo wa kuchinjilia tu pasipo kuangalia aliyeongoza alikuwa Waziri wako au Nani.

Kwa kufanya hivyo,nakuhakikishia utajiongezea imani kubwa kwa wananchi na utakuwa umewafunza adabu wanaCCM wote wenye hayo mambo ukianzia na viongozi wako wa chama ngazi za chini.

Nimalizie kwa maombi haya mawili:-

1. Baada ya uchaguzi,naomba uwepo utaratibu maalumu wa Mara kwa mara wa kutoa elimu ya uraia kwa wanachama wote hasa ya RUSHWA.Maana Hawa wanachama nao ni chanzo kikubwa Cha kushawishi wapewe rushwa kwamba eti kura hawampi asiyewapa bahasha.

2. Naomba katiba ya CCM irekebishwe kipengele Cha mwenyekiti wa CCM taifa ili Si lazima Rais awe mwenyekiti wa chama.Nina imani hili likifanyika,utaisafisha CCM kuwa chama Safi na kuliko hivi Sasa inavyoonekana CCM na RUSHWA ni Kama BABA na MWANA.

TUNASUBIRI KWA HAMU UTUSHANGAZE.
 
Back
Top Bottom