Hongera Rais Magufuli kwa kunusa uvamizi unaofanyika Ndachi Nkuhungu, Dodoma

Hongera Rais Magufuli kwa kunusa uvamizi unaofanyika Ndachi Nkuhungu, Dodoma

bulicheka 4

JF-Expert Member
Joined
Mar 22, 2020
Posts
915
Reaction score
1,019
Jana Mh Rais akiwa eneo la Kizota ukifungua nyumba za askari wa Magereza ulitamka kuna eneo wananchi wanafukuzwa na mapanga.

Ni kweli kabisa. Cha ajabu uongozi umekaa kimya na kuwapa wababe wenye silaha kuzidi kumega ardhi za wamama wajane na wakongwe waliostaafu.

Ardhi kwa maelekezo hati zao za miaka 33 zimekwisha muda. Kudai eneo wamenyang'anywa linapimwa upya na kugawiwa waliovamia na kujenga.

Tunaomba Mh Rais pua yako inuse zaidi
 
Raisi wa wanyonge msikivu na mwenye huruma ndio maana tulimpigia kura za funga kazi na ziada ili zikipungua aongeze,amekusikia atafanyia kazi!
 
Mbunge analo eneo block f"ila sarakasi aliyo tuchezea ni Mungu anaju na hakika pua za Rais zitajua

Inashangaza Mh Rais kuwalipa bila kuwadhulumu Ihumwa,Michese watu walio pitiwa na reli mpya ambao walikuwa wana miliki ardhi kimila iweje Wavamizi wasiwalipe wamiliki Halali ambao hata Mh Rais alipoingia madarakani alielekeza hati zote Dodoma zihuishwe ziwe miaka 99 kama Sengerema na kwingineko

Tunasubiri tumsikie Waziri akumbuke alipojenga nyumbayake Kijijini Iringa alituonyesha mfano wa kutii sheria bila shuruti
 
Raisi wa wanyonge msikivu na mwenye huruma ndio maana tulimpigia kura za funga kazi na ziada ili zikipungua aongeze,amekusikia atafanyia kazi!
Mwambie kwanza aache dhuluma dhidi ya watumishi wa umma! Haiwezekani tangu watu waajiriwe mwaka 2014, mpaka leo hawajapandishwa madaraja yao.

Rais wa wanyonge hawezi kuwa mkatili, mwonevu, mbinafsi, mkaidi na mwenye hulka ya kupenda kujitweza, kutukuzwa na kuabudiwa!
 
Utumishi wa Umma,siyo sehemu ya kujipatia utajiri!! By Mwalimu JKN!!
 
Utumishi wa Umma,siyo sehemu ya kujipatia utajiri!! By Mwalimu JKN!!
Kupanda madaraja/cheo ni haki ya mfanyakazi yeyote yule duniani kutoka kwa mwajiri wake. Lengo ni kumuongezea morali na ari ya kufanya kazi kwa bidii na maarifa zaidi.

Unapo mdhulumu mfanyakazi haki yake kwa makusudi, unampunguzia morali na hiyo ari ya kufanya kazi kwa ufanisi zaidi. Matokeo ya huu uonevu, ni kwa mfanyakazi huyo kufanya kazi chini ya kiwango, kutotimiza wajibu wake ipasavyo, nk.
 
Kupanda madaraja/cheo ni haki ya mfanyakazi yeyote yule duniani kutoka kwa mwajiri wake. Lengo ni kumuongezea morali na ari ya kufanya kazi kwa bidii na maarifa zaidi.

Unapo mdhulumu mfanyakazi haki yake kwa makusudi, unampunguzia morali na hiyo ari yakufanya kazi kwa ufanisi zaidi. Matokeo ya huu uonevu, ni kwa mfanyakazi huyo kufanya kazi chini ya kiwango, kutotimiza wajibu wake ipasavyo, nk.
Kupandisha kila Mwaka Mishahara,nako kuna ongeza sana Mfumuko wa bei na kushusha thamani ya shiling! Tuvumulieni muda si mrefu mtaona shiling yetu inavyopanda thamani, Mtu hata akilipwa laki tano ataona thamani yake!!
 
Mwambie kwanza aache dhuluma dhidi ya watumishi wa umma! Haiwezekani tangu watu waajiriwe mwaka 2014, mpaka leo hawajapandishwa madaraja yao.

Rais wa wanyonge hawezi kuwa mkatili, mwonevu, mbinafsi, mkaidi na mwenye hulka ya kupenda kujitweza, kutukuzwa na kuabudiwa!
Mkuu, waachie liutumishi lao la umma nenda kajiajiri. Unakaa unalialia mchana kutwa, hujui kuwa kuna mamilioni ya watu wako vijiweni hawana hata hiyo ajira ya utumishi wa umma. Kama wanawazingua, toka nenda kwenye sekta binafsi au kaanzishe kilimo cha kisasa, kinalipa.
 
Kupandisha kila Mwaka Mishahara,nako kuna ongeza sana Mfumuko wa bei na kushusha thamani ya shiling! Tuvumulieni muda si mrefu mtaona shiling yetu inavyopanda thamani, Mtu hata akilipwa laki tano ataona thamani yake!!
Kilio cha Wafanyakazi wengi wa nchi hii kwa sasa siyo kupandishiwa mishahara kila mwaka kama unavyodai!! Wafanyakazi wanadhulumiwa haki zao na Rais aliyeko madarakani mchana kweupe.

Tangu alipoingia madarakani, alisitisha upandaji wa madaraja/cheo cha muundo kwa wafanyakazi kwa utaratibu wa kila miaka mitatu kwa kisingizio cha kufanya uhakiki kwa watumishi hewa na wale wenye vyeti feki.

Baada ya hapo akaanza visingizio vya kununua ndege na pia kuwataka wafanyakazi kusubiri mpaka amalize muda wake wa utawala.

Huu ni uonevu na dhuluma kwa wafanyakazi. Leo hii mafanyakazi aliyeajiriwa mwaka 2014, amepitwa kiwango cha mshahara na yule aliye ajiriwa mwaka 2020 kwa daraja lile lile. Mambo haya hayakuwepo enzi za JK.

Lakini bado uonevu huu unawaathiri hata wale wafanyakazi wanao karibia kustaafu! Wanajikuta wanapokea pensheni ambayo haiendani na daraja ambalo mstaafu angestahili.

Wafanyakazi tunataka utaratibu wa madaraja urudishwe. Huu uonevu unao endelea, unatukatisha wengi tamaa ya kufanya kazi kwa moyo.
 
Mkuu, waachie liutumishi lao la umma nenda kajiajiri. Unakaa unalialia mchana kutwa, hujui kuwa kuna mamilioni ya watu wako vijiweni hawana hata hiyo ajira ya utumishi wa umma. Kama wanawazingua, toka nenda kwenye sekta binafsi au kaanzishe kilimo cha kisasa, kinalipa.
Kukimbia tatizo siyo njia sahihi. Dawa ya tatizo ni kulikabili. Mimi hapa nilipo nilishajiongeza kitambo. Lakini bado nina wajibu wa kudai haki yangu kutoka kwa mwajiri.

Tukisema wote tujiajiri, ni nani atakaye toa huduma kwa wengine? Ni jukumu letu kuwajibika kufanya kazi kwa bidii, lakini pia ni wajibu wa mwajiri kutenda haki kwa waajiriwa wake.

Kuhusu hao wahitimu walio mtaani, ni wajibu wao nao kuipigia kelele serikali iwaajiri. Kuishi kwa kusubiria sisi tuache kazi kwa sababu ya hasira, bado hakuwezi kuwa ni suluhisho la haraka kwao.
 
Back
Top Bottom