Hongera Rais Samia Suala la Uwekezaji Nchini

Hongera Rais Samia Suala la Uwekezaji Nchini

Amosi Mgonja

Member
Joined
May 15, 2021
Posts
5
Reaction score
5
HONGERA MAMA SAMIA KWA MPANGO WA MAPITIO YA SHERIA 22 KUBORESHA MAZINGIRA YA BIASHARA NA UWEKEZAJI NCHINI

Serikali ya Tanzania chini ya uongozi wa Mh.Rais Samia Suluhu Hassan iko katika mchakato wa kushirikisha wadau mbalimbali katika kufanya mapitio ya sheria 22 chini ya Wizara ya Viwanda na biashara ili kuweza kuboresha mazingira ya biashara nchini. Maboresho haya yataibua fursa kwa sekta binafsi na kuvutia wawekezaji zaidi.

Mpango wa uboreshwaji wa sheria katika Wizara hii muhimu ni muendelezo wa jitihada za Mh.Rais kuimarisha sekta zote ili kujenga uchumi imara na shindani. Mpaka sasa vikao mbalimbali vya kisekta vimefanywa katika wizara zote muhimu kwa kushirikisha wadau ili kuweza kuimarisha mazingira ya biashara na uwekezaji nchini.

Makusanyo ya kodi, fursa za ajira, maendeleo ya teknolojia, ni baadhi ya faida zitakazotokana na jitihada zinazofanywa sasa katika kuimarisha mazingira ya biashara uwekezaji nchini. Kongole Rais Samia kwa kuona haja ya kuboresha sekta hii muhimu, KAZI IENDELEE
 
Back
Top Bottom