Mkuu,
Pongezi kwa uongozi wa RT na pia mdau kwa kuleta huu uzi Jamiiforums .
Habari hii ya gazeti la Ippmedia ina upungufu mkubwa, haibainishi wanariadha hawa watashindana ktk mbio urefu gani Marekani, kwa mfano kama ni marathon ili kukubaliwa ktk mashindano makubwa mkimbiaji anatakiwa kuwa na rekodi binafsi bora (best personal time) ya angalau 2hrs :12 minutes 00 seconds .
Waandishi wa habari wajitahidi kufahamu hao wakimbiaji wetu wameshiriki mashindano gani ya nyumbani iwe za majeshi n.k na ubora wao ktk kumaliza mbio husika ili kukuza hamasa za washabiki na wale wengine wenye tamaa ya kujihusisha na riadha ili kukuza mchezo huo.