Hongera Sabaya kwa kufunua ukweli, pengine wasiojulikana watajulikana

Hongera Sabaya kwa kufunua ukweli, pengine wasiojulikana watajulikana

Gift mzalendo

JF-Expert Member
Joined
Dec 13, 2019
Posts
1,856
Reaction score
2,417
Kwa kifupi Sabaya amefunua ukweli ambao wengi tusingeweza kuufahamu kirahisi.

Kwanza ni ujasiri mkubwa kuwataja viongozi wakubwa kwenye kesi ambayo inaonyesha Kuna uhalifu, Kukiri kwamba alitumwa na mamlaka ya uteuzi ni dhahiri kwamba kuna uwezekano kwamba nayo ilihusika.

Wengi tunafamu vitendo vingi viovu vilivyofanywa na watu ambao tuliambiwa hawajulikani mpaka leo, pamoja na kuwa na Jeshi la polisi na vitengo vya upelelezi. Ikizingatiwa pia baadhi ya vitendo hivyo viliacha ushahidi wa kutosha kama video, CCTV, finger print nk

Kwa vile amekiri kwamba kuna matukio mengine mengi amefanya kwa staili hiyo, nashauri apewe nafasi ya kuelezea matukio yote aliyoyafanya ili yachunguzwe , tunaweza kubaini Mambo mengi yasiyojulikana.
 
Wao walijichanganya kumfukuza kazi alaf kuruhusu kudhalilishwa kwake , huku wakijua ukweli wote , Kibaya Zaid hawaonyeshi kumsaidia, tulionya Sana humu kuwa kijana asiwe mbuzi wa kafara wakat kiuhalisia aliwekwa pale Hai kimkakati....ni Sawa na leo Mstaaf wa DSM ashitakiwe alaf mamlaka wajitenge , akibanwa anayamwaga yote
 
nilichoelewa hapa nafasi za urais zimepelekea sabaya aropoke hivo, namanisha waliomfata kumwona selo ndio wamemdanganga amuharibie MPANGO
 
Hapa napata picha kumbe hata waliompiga risasi Tundu Lissu walitumwa na mamlaka za uteuzi. Nimeelewa ile kauli aliyotoa Sabaya siku anakamatwa kuwa wakati ukifika atamtaja anayeendesha karakana ya ibilisi. Asante Sabaya kutufumbua macho
Kwahiyo kaisha maliza mchezo kumtaja[emoji1787][emoji1787][emoji1787].jiwe alikua sio binadamu wa kawaida
 
Hivi angetuma ujumbe kwa viongozi wa juu wa CCM, kujishusha na kuomba msamaha na kupewa adhabu ndogo(kama itashindikana kuachiwa huru) nafikri hii kesi ingemwendea vizuri. Mahakama ni tawi la CCM, hawashindwi kitu wakiamua na hakuna wakuwahoji.
 
Back
Top Bottom